Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Chwaka Stars na JKU Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU Imeshinda 2--1.

Kizaazaa katika goli la timu ya Chwaka stars wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan unguja timu ya JKU imeshinda kwa bao 2--1
 Vitendo vya imani ya ushirikina katika michezo vimeshamiri kama inavyoonekana hapa likiwa limevunjwa yai jirani na kibendera cha kona.


 Mshambuliaji wa timu ya JKU akimpita beki wa timu ya Chwaka Stars wakati wa mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan Timu ya JKU imeshinda 2--1.
Viongozi wa Timu ya Kijichi wakifuatilia mchezo kati ya Chwaka Stars na JKU uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa bao 2--1.


 Wachezaji wa Timu ya JKU wakishangilia bao lao la Pili na la ushindi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.