Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein Azungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Dimani Unguja.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa UWT Wilaya ya Dimani baada ya kuwasili katika viwanja vya Tawi la CCM Kiembesamaki kuzungumza na viongozi hao. katika ukumbi huo

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wa meza kuu wakisimaa kwa dakika moja kumuombea dua Mbunge wa Jimbo la Dimani Marehemu Hafidh Ali Tahir kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Tawi la CCM Kiembesamaki Unguja.

Viongozi wa UWT Wilaya ya Dimani Kichama wakisimama kwa dakika moja kumuombea dua aliyekuwa Mbunge wao aliyefariki hivi karibuni. akiwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Marehemu Hafidh Ali Tahir.

Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Kichama Bi Zuwena Suleiman Mohammed akisoma risala ya UWT kwa mgeni rasmin.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dimani Bi Khadija Kassim Shamte akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin kuzungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Dimani katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa tawi la CCM Kiembesamaki Unguja.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.