Habari za Punde

Mwekezaji Pemba alala Rumande, Zaeca wataka sheria ifuatwe

Na mwandishi wetu - Pemba.
Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (Zanzibar Anti-Corruption And Economic Crimes Authority - ZAECA) imesema kua imejipanga kikamilifu kupambana na wale wote wanaojishuhulisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi huku ikisema kua hakuna atakaekwepa mkondo wa sheria iwapo atakwenda kinyume na sheria zilizowekwa nchini.
Hayo yameelezwa na Mdhamini wa mamlaka hiyo Pemba Nd: Suleiman Ame Juma wakati alipokua akizingumza na mwandishi wa habari hizi afisini kwake chakechake Pemba kufuatia tukio la kumkamata mwekezaji wa hoteli ya kitalii inayotambulika kwa jina la THE AIYANA iliyopo Makangale mkoa wa kaskazini Pemba.
Mdhamini huyo amesema kua, kumekua na baadhi wa wafanya biashara wasio waaminifu wanakwepa kulipa kodi nchini na hatimae kuikosesha serikali mapato yake, amesema ZAECA imejipanga vyakutosha kukabiliana na wafanyabiashara wa aina hiyo.
Akizungumzia tukio hilo la leo la kukamatwa mwekezaji wa hoteli hiyo bw: Naraindra Sungkur raia wa Mauritius amesema kua , mwekezaji huyo wamemkamata kwa makosa ya kushindwa kulipa kodi ya ardhi 2014/2015 na 2015/2016 na deni analodaiwa ni $D 40,200 kwa makisio ni sawa na 88,440,000 (milioni themanini na nane laki nne na arubaini elfu)
Juma amefahamisha kua, mara baada ya kupata taarifa hiyo, mamlaka iliamua kumwandikia hati ya wito na iliandika hati hizo zisizopungua tatu lakini hakutii amri hiyo ambapo amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria kwa mujibu wa sheria ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi zanzibar
“kwa vipindi tofauti tumemwandikia hati hizo lakini hakuna hata moja aliyotoa mashirikiano, ya kwanza ilikua 12/04/2016 hakuitika, pia 27/05/2016 hakuitika , isitoshe tena 22 /06/2016 pia alipinga wito huo, hivyo leo tumeamua rasmi kwenda kumkamata na kumsomea tuhuma hizo na baadae kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na wao wameridhika na ushahidi na hatimae kumpeleka Mahakamani ” alisema Juma
Aidha Mdhamini huyo amesema kua, mara baada ya kumkamata waliwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na kuliwasilisha jalada la mtuhumiwa huyo, pasi na kumchelewesha baada ya taratibu hizo kukamilika walimpeleka mahkamani na kosa lake limesomwa na mahkama ya mkoa, hivyo mahkama hiyo haikuweza kumpatia dhamana kwasababu kisheria haina uwezo wa kusikilisha shauri hilo, hivyo mtuhumiwa amewekwa rumande mpaka pale kesi yake itakaposomwa tena 05 /12/ 2016.
Kwa mara nyengine mdhamini huyo amerejelea kauli yake kwa wawekezaji nchini akiwataka kufuata na kuheshimu sheria zilizowekwa ili kujiepusha na misukosuko inayoweza kuepukika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.