Habari za Punde

Michuano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 Kati ya Wilaya ya Kati Unguja na Wilaya Magharibu A Unguja, Yanayofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mshambuliaji wa Timu ya Wilaya ya Magharibu A Unguja Mohammed Faraji akimpita beki wa Timu ya Wilaya ya Kati Unguja  Issa Mohammed wakati wa mchezo wao wa kuwania Ubingwa wa ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bila ya kufungana na mshindi akapatikana kwa njia ya Penenti Timu ya Magharibi A imeshinda kwa penenti 7-6. mMichuano hiyo imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC ) ili kuinua vipaji vya Watoto katika mchezo wa mpira Zanzibar. Michuano hiyo inashirikisha Timu kutoka Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kikosi cha Timu ya Wilaya ya Magharibi A Unguja imefanikiwa kusonga mbele kuingia Robo fainali ya Michuano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 kwa kuwafunga kwa penenti Timu ya Wilaya ya Kati Unguja kwa Penenti 7-6
Kikosi cha Timu ya Wilaya ya Unguja kilichotoa upinzani kwa Timu ya Wilaya ya Magharibi A katika michuano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17. kwa kukubali kipigo cha mikwaju ya penenti 7-6.
Mshambuliaji wa Timu ya Wilaya ya Magharibi A Unguja mwenye jezi nyeupe akimpita beki wa Timu ya Wilaya ya Kati Unguja wakati wa mchezo wao wa Kombe la ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Magharibi imeshinda kwa penenti 7-6
Kocha wa Timu ya Magharibi A Unguja akitowa maelekezo kwa wachezaji wake 
Jopo la mocha wa Timu ya Wilaya ya Kati Unguja wakitowa maelekezo kwa wachezaji wake mpira uliposimama kwa kutowa huduma ya kwanza kwa mchezaji aliyepata majaraha mchezoni akipata huduma ya kwanza uwanjani. 

Watatibu wa Michuano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup Maofisa wa ZBC wakifuatilia michuano hiyo kwa makini kuona wapi yapo mapungufu ili kuweza kurekebisha. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.