Habari za Punde

Shamrashamra za Kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar Yaanza kwa Michezo wa Nage Zanzibar.

 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Hamad Yussuf Masauni akipokea Maandamano ya Wanamichezo wa Mchezo wa Nage Zanzibar Jumla ya Timu 32 Zinashiriki michuano hiyo ya kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwa na Viongozi wa Jimbo las Kikwajuni na Mkurugenzi wa Radio Coconut FM Ndg Ali Dai, michuano hiyo ya Nage imeandaliwa na Kituo cha Redi cha Coconut FM Zanzibar. 
Timu ya Watangazaji na Waandishi wa Redio Coconut FM waandalizi wa Michuano hiyo ya Nage Zanzibar kuadhimisha Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, michuano hiyo inafanyika katika viwanja vya Tumbatu Miembeni Zanzibar. 
Washiriki wa michuano ya Mchezo wa Nage wakipita mbele ya mgeni rasmin wakati wa ufunguzi wake uliofanyika katika viwanja vya tumbaku miembeni Zanzibar jumla ya Timu 32 zinashiriki michuano hiyo ilioandaliwa na Kituo cha Redio cha Coconut FM Zanzibar.
Washiriki wa michuano ya Nage walipita mbele ya mgeni rasmin.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.