Habari za Punde

Akina Mama Waifagilia Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mbunge viti maalumu CCM Mkoani Mwanza, Mkuu wa Mo Dewji Foundation, Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza pamoja na wadau wengine, wakiwa kwenye wodi ya akina mama hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, kujionea hali ya wodi hiyo.
Na.LakeFmHabari
Baadhi ya akina mama waliojifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wameishukuru serikali pamoja na wadau wengine wa afya kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

Akina mama hao wameyasema hayo jana baada ya mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, kukabidhi msaada wa vitanda, magodoro, mashuka na vyandarua katika hospitali hiyo.

Wamesema hivi sasa huduma za afya hususani kwa mama na mtoto zimeboreshwa katika hospitali hiyo ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo wameomba maboresho zaidi yaendelelee ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza huku msisitizo ukiwa ni kuwahamasisha akina mama kujifungulia kwenye vituo vya afya.

Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota kwa kushirikiana na taasisi ya Mo Dewji amesaidia upatikanaji wa mashuka 100 pamoja na vitanda 20 vilivyoambana na magodoro pamoja na vyandarua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.