Mbunge wa Jimbo
la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wasanii maarufu
wa kizazi kipya kutoka Tanzania Bara na Visiwani kabla ya Wasanii hao kupanda
jukwaani kutoa burudani katika Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
2016-2017 yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Mhandisi Masauni ili kukuza vipaji vya
vijana. Picha zote na Felix Mwagara.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akiwasalimia wachezaji
wa Karakana City wakati akikagua timu za mchezo wa Nage zilizoingia Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi
CUP 2016-2017. Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia
ni naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo
mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo yaliyofanyika
katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar.
Katika mashindano hayo,
timu ya Six Centre iliibuka mshindi dhidi ya timu ya Karakana City zote za
mjini Unguja.
Picha zote na
Felix Mwagara.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza na mamia
ya wananchi waliouhudhuria katika Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, ambaye ndiyo mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga
Mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Kulia
ni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.
Hamisi Kigwangala. Katika mashindano hayo, timu ya Six Centre iliibuka mshindi
dhidi ya timu ya Karakana City zote za mjini Unguja. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge wa Jimbo
la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (wapili kulia) kuja kufunga
Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 katika Uwanja wa Amani,
mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba yake Masauni ambaye ndiyo aliyeandaa
msahindano hayo alisema, mchezo huo utazidi kuthaminiwa ili kuwaweka vijana
pamoja. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge wa Jimbo
la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akiwa katika picha ya pozi na Msanii wa nyimbo za Singeli,
Manfongo kabla ya msanii huyo kupanda jukwaa kutoa burudani katika Fainali za
Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017, yaliyofanyika katika Uwanja wa
Amani, mjini Unguja Zanzibar. Wasanii mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani
walitoa burudani katika fainali hiyo ambapo timu ya Six Centre iliibuka kidedea
dhidi ya Karakana City, zote za mjini Unguja. Mashindano hayo yaliandaliwa na
Mhandisi Masauni ili kukuza vipaji vya vijana.
Picha na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment