Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, akimpokea Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (Mbunge wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar),
wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza
la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally, akiwaongoza
wajumbe wengine wa kamati hiyo kusalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza
wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na
Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, Jijini Mbeya
Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kulia), akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo
ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wakwanza kulia), kuingia
ndani ya Gereza la Kilimo la Songwe,lililopo wilayani Mbalizi, jijini
Mbeya, ambapo wajumbe wa kamati walipata
fursa ya kusikiliza maoni kupitia risala
iliyoandaliwa na wafungwa wa gereza hilo.Wengine ni viongozi wa gereza hilo
Afisa wa Jeshi la Magereza akijibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea shamba la mahindi linalomilikiwa na
Gereza la Kilimo la Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya.Wa kwanza
kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu
maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya
kutembelea shamba la Mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo Songwe, lililopo
wilayani Mbalizi, jijini Mbeya.
(Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment