Habari za Punde

Shamra shamra wa Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba Kuadhimisha Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimiana na wananchi kisiwa Cha Mwambe Shamiani baada ya kuwasili katika kisiwa Hicho, kwa ajili ya Uzinduzi wa mradi wa Umeme katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akikunjuwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa Umeme katika Kisiwa cha mwambe Shamiani Wilaya ya Chake Chake, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 AFISA Mdhamini Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Pemba, Juma Bakari Alawai, akitoa taarifa ya Kitalaamua katika uzinduzi wa mradi wa Umeme katika kisiwa cha Mwambe Shamiani Wilaya ya Mkoani, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na wananchi wa Kisiwa Cha Mwambe Shamiani Wilaya ya Mkoani, baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Umeme katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar, Mh:Mohamed Aboud Mohamed, akikunjuwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya Baraza la maji Chake Chake, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Salama Mbarouk Khatib na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akibadilishana mawazo mara baada ya kufunguliwa kwa Ofisi ya Baraza la Mji Chake Chake, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 KATIBU mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ, Radhia Rashid akizungumza na wananchi wa Chake Chake mara baada ya kufunguliwa kwa Ofisi ya Baraza la mji Chake Chake, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majidi Abdalla, akizungumza na wananchi wa Chake Chake mara baada ya kufunguliwa kwa ofisi ya Baraza la Mji Chake Chake, katika Shamra shamra za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Habiba Zarali, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.