Habari za Punde

Yaliojiri Wakati wa Kutangazwa Mshindi wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Dimani Zanzibar.

 Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC Wilaya ya Magharibi Unguja Bi Fatma Gharib akitangaza matokea ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar katika Ofisi za Tume zilioko katika Skuli ya Sekondari Kiembesamaki Zanzibar baada ya kukamilika taratibu zote za Kisheria za Uchaguzi na kupatikana mshindi wa Uchaguzi huo mdogo uliofanyika katika jimbohilo baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbohilo Mhe Hafidh Ali Tahir kufariki dunia mwaka jana.
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Ndg Ali Juma Ali, akiwa katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki akifuatilia matekeo ya Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo la Dimani akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja Ndg Yussuf Mohammed wakifuatilia matokeohayo. 

 Mshindi wa kinyanganyirocha kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbola Dimani Ali Juma Ali akitia saini fomu ya matokeo baada ya kutangazwa na tume kushinda uchaguzi huo.

Mshindi wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar Ndg Ali Juma Ali akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo na kuwaahidi Wananchi wa Jimbo la Dimani kujiandaa na maendeleo ya jimbo lao na kuendeleza maendeleleoa yaliazishwa na marehemu Hafidh Ali Tahir.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.