Habari za Punde

Afariki katika ajali ya boti Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Rashid Leja mkaazi wa Mambasa Kenya mwenye umri wa miaka 25 amefariki dunia baada ya chombo alichokuwa akisafiria kupingwa na wimbi na kupelekea kuzama kwa chombo hicho.

Akithibitisha kutokea kwa tokeo hilo kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji amekiri kupokea mwiili wa nd Rashid Leja ambaye tayari ameshafariki dunia .

Amesema kifo cha nd Rashid Leja kimesababishwa na kuzama kwa chombo alichokua akisafiria kilichokuwa kikitokea Mambasa Kenya na kuja kisiwani Pemba .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya wete, Rashid Hadidi Rashid amesema ajali hiyo imetokea eneo la kisiwa cha Fundo Wilaya ya wete mkoa wa kaskazini Pemba ambapo imesababishwa na manahodha kutokana na kufanya uhaulishaji wa abiria kwa kuwaingiza katika chombo chengine na kupelekea abiria hao kuzama baharini na mmoja kufariki dunia .

Aidha amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya manahoza hao ambao wamesababisha ajali hiyo .

Nae afisa bandari katika wilaya ya wete nd Hassan Hamad amesema chombo hicho kilichosababisha ajali hakina hakina ruhusa ya kuchukua abiria bali kinaruhusa ya kuchukua mizigo pekee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.