Habari za Punde

Wakulima Pemba wakabidhiwa matenki ya kuhifadhia maji na mipira maalum ya umwagiliaji

 BAADHI ya vifaa (matangi) kwa ajili ya kuhifadhi maji kwa wakulima na wanavikundi vya ushirika, vya mboga mboga na migomba vya wilaya nne za Pemba, waliokabidhiwa na Mkuu wa Program ya Kilimo na Kuimarisha Mifugo ASSP Zanzibar dk Talib Saleh Suleiman, hafla iliofanyika afisi za ASSP Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 BAADHI ya wakulima na wanaushirika wa mboga mboga na migomba kutoka mikoa miwili ya Pemba, wakisikiliza hutuba kwenye hafla ya kukabidhiwa, matenki ya kuhifadhia maji na mipira maalumu kwa ajili ya umwagiliaji kwa njia ya matone, hafla iliofanyika ofisi ya ASSP Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nasso, Pemba).
 MKUU wa Mradi wa kuimatisha kilimo na ufugaji Zanzibar ASSP dk Talib Saleh Suleiman, akizungu na wanaushirika na wakulima mmoja mmoja wanaojishughulisha na kilimo cha mboga mboga na migomba, kabla ya kuwakabidhi mipira na matangi ya kuhifadhia maji kwa ajili ya kilimo chao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mradi wa Kuimatisha Kilimo na Ufugaji Zanzibar ASSP dk Talib Saleh Suleiman (kulia), akimkabidhi mkulima wa mboga mboga Msanifu Ali Faki tangi lenye ujazo wa lita 1000 na mipira seti mbili, kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji MAJI kwa njia ya matone, hafla hiyo ilifanyika Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mradi wa Kuimatisha Kilimo na Ufugaji Zanzibar ASSP dk Talib Saleh Suleiman (kulia) akiwakabidhi viongozi wa ushirika wa ‘mwisho wa ubaya’ uliopo Chakechake mipira seti mbili kwa ajili umwagiliaji na tanki la lita 5,000 la kuhifadhi maji, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mradi wa Kuimatisha Kilimo na Ufugaji Zanzibar ASSP dk Talib Saleh Suleiman (kulia), akimkabidhi mkulima wa mboga mboga Said Salum Mussa tangi lenye ujazo wa lita 1,000 na mipira seti mbili, kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji  maji kwa njia ya matone, hafla hiyo ilifanyika Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MWANDISHI wa Gazeti la Zanzibar Pemba Haji Nassor, akizungumza na mwanaushirika wa ‘wengi si hoja’ wa Kiwani Bihawa Burhan Hamad wanaojishughilisha na kilimo cha mboga mboga, muda mfupi baada ya kukabidhiwa mipra kwa ajili ya umwagiliaji kwa njia ya matone, (kwa hisani ya TSJ-Pemba)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.