Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Timu ya JKU na Chuoni Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU Imeshinda 3-2.

Mshambuliaji wa Timu ya JKU wakiwapita walinzi wa Timu ya Chuoni wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda bao 3-2.

 Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani na mashambulizi ya kwa kila upandade kumshambulia mwezanke katika dakika ya 30 ya mchezo huo kipindi cha kwanza mchezani wa timu ya Chuoni ameiandikia bao la kwanza lililofungwa na mchezaji Hafidh Juma. goli hilo limedumu kwa dakika 6 za mchezo huo katika kipindi cha kwanza.

 JKU imepata bao la kusawazisha katika dakika ya 36 ya mchezo huo kipindi cha kwanza kupita mfungaji wake Khamis Abdallah ameiandikia bao la kusawazisha timu yake hadi mapumziko timu hizo zimekuwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili cha mchezo huo kilikuwa cha timu ya JKU na kupata bao lake la pili kupitia mfungaji wake Shomar Waziri ameiandikia bao la pili timu yake katika dakika ya 66, Timu ya Chuoni ilifanya kazi ya ziada kuandika bao la kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Abrahaman Mbarouk ameiandikia bao katika dakika ya 87 ya mchezo huo. 

Timu ya Chuoni haijaka vyema ilipachikwa bao la tatu na la ushindi kwa timu ya JKU kupitia mchezaji wake Suwedi Juma katika dakika ya 89 ya mchezo huo kipindi cha pili hadi mchezo huo unamaliziki timu ya JKU imetoka na ushinda wa mabao 3-2. 











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.