Habari za Punde

Ligu Kuu ya Zanzibar Ikiendelea Katika Uwanja wa Amaan Kati ya JKU na Miembeni Timu ya JKU Imeshinda Bao 1-0.

Benchi la Ufundi la Timu ya Miembeni wakiwa na simazi baada ya kupoteza mchezo wao huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Timu ya JKU mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU akipiga mpira golini kwa timu ya miembeni huku kipa wa timu hiyo kushindwa kuuzuiya mpira huo. 
Kipa wa timu ya miembeni akiwa katika jitihada za kuokoa mpira huo bila ya mafanikio huku beki wake akiwa tayari kutowa msaada. 
Beki wa Timu ya Miembeni akiokoa mpira huo kabla ya kufika nyavuni. baada ya kumpita kipa wa timu hiyo wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa amaan timu ya JKU imeshinda bao 1-0. 


 Wachezaji wa Timu ya JKU wakiomba dua baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar kumalizika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Miembeni. 
Jopo la Wazee wa Timu ya Miembeni wakitafakari baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar kumalizika kwa timu yao kufanya vibaya katika mchezo huo kwa kukubali kufungwa na Timu ya JKU mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.