Baskeli ni moja ya usafiri mkubwa katika mji wa Zanzibar na Vitongoji vyake unaotumiwa na Wananchi wa Zanzibar tangu enzi hizo ulikuwa ni mkubwa na wazee wa zamani walikuwa wakiziita gari kwa kuwarahisishia usafiri wa kwenda kazini na mashambani.Bado usafiri huo hutumika katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa miaka hii watumiaji wakubwa na wanafunzi wa maskuli kwa usafiri wa kwenda na kurudi skuli.
Kama zinavyoonekana baskeli hizo zikiwa nje ya majengo ya Skuli ya Unguja Ukuu, Kaepwani, Wilaya ya Kati Unguja.
Usafiri wa daladala hutumika na watu wengi katika maeneo ya Manispaa ya Zanzibar kwa kuwarahisishia kufika kwa haraka safari zao wakati wote wa matembezi yao na shughuli nyengine.
Lakini kuna baadhi ya madereva wa daladala hutumia gari hizo kwa kukimbizana kutaka kuwahi katika kituo cha daladala kuwahi kuchukua abiria bila ya kujali usalama wa abiria wao kama inavyoonekana pichani gari hizi zikishindana kupita katika raundi abauti ya Michenzani kuwahi kuchua abiria bila ya kujali usalama wa abiria wao.
No comments:
Post a Comment