Marriott
International Inc.ni kampuni ya Kimarekani inayomiliki hoteli nyingi za kimataifi katika kila pande ya dunia.Katika jitihada za kuongeza umaarufu
wake,mwezi Septemba mwaka 2016 Marriott International Inc., ilinunua Hoteli za
Star wood kwa gharama ya dola za Kimarekani bilioni kumi na tatu.
Pia mwaka 2014 Marriott
International Inc ilifanikiwa kununua Protea Hospitality Group toka Afrika Kusini kwa dharama za dola za Kimarekani bilioni mbili.
Kwa manunuzi hayo Marriott International Inc., imekuwa ndio mmiliki mkubwa kuliko wote duniani ikiwa na jumla ya vyumba vya kulala wageni milioni moja nukta moja
(1.1m) duniani kote.
Marriott
International Inc. kwa sasa ipo katika mazungumzo ya mwisho na Pennyroyal Gibraltar
Ltd kuhusu ujenzi wa Hotel ya Ritz Carlton Zanzibar ambayo itakua ndani ya Zanzibar
Amber Resort.
Rais wa hoteli za Marriott
Mashariki ya Kati na Afrika Bwana.Alex Kyriakidis ametembelea kisiwa cha Unguja na kukutana na wadau wa sekta ya utalii pamoja na viongozi wa serikali ya
Zanzibar ili kujionea mazingira na kupata uelewa wa jinsi mradi huu utakavyoendelezwa hapa
Zanzibar .
‘Ni metegemeo yetu kuwa ujenzi wa Hoteli ya
Ritz Carlton utachochea ongezeko la watalii ndani ya kisiwa cha Zanzibar na kukuza uchumi
wake kwa ujumla.’ alisema Bw. Kyriakidis.
Ritz
Carlton, ambayo inamilikiwa na Marriot International Inc.inamiliki hoteli moja tu barani Afrika iliyomo Cairo- Misri,
na inategemea kuongeza matawi yake kisiwani Zanzibar kupitia Zanzibar Amber Resort.
Ritz Carlton Zanzibar Hotel itajengwa katika usanifu wa kipekee kwenye eneo la ufukwe wa Bahari ya
Hindi kaskazini mashariki mwa kisiwa hicho.
katika harakati za kupanua wigo wake barani Afrika na kuleta uzoefu wake wa miaka mingi kwenye fani ya hoteli ndani ya
Zanzibar. Ritz Carlton inaamini kuwa Zanzibar inauwezo mkubwa wa kukuza uchumi wake kupitia utalii,na nifuraha kubwa katika miongoni mwa kampuni inayochochea na kusaidia ukuwaji huo.’
No comments:
Post a Comment