Habari za Punde

Micheweni ilivyoweza kunufaika na utalii

Na Abdi Suleiman, PEMBA.


PEMBA peremba ndivyo baadhi ya watu wanavyopenda kuita, Pemba ya miaka 50 iliyopita ya Kikoloni sio Pemba ya leo, ambayo inaonekana kuwa imebadilika.

Kwa kiasi kikubwa kila mtu hawezi kuamini nini kilichoifanya Pemba,wa katika hali hii iliyopo imepiga hatua kubwa kimaendeleo, majengo marefu ya ghorofa, mahoteli mbali mbali ya kitalii yenye hadhi kubwa sana tu yapo Pemba.

Kwa muda mrefu kisiwa Cha Pemba kimekuwa kikisifika kwa ukulima wa zao la Karafuu, ambalo limekuwa likitegemewa sana kwa kuipatia nchi pesa nyingi za kigeni baada ya kuuzwa nje.


Sasa Pemba imanza kuimarika na kupata sifa kubwa sana kupitia sekta ya Utalii, unapotaja utalii moja kwa moja unalenga Wilaya ya Micheweni, ambayo imekuwa ikiongoza kwa utalii kutokana na kuwa na vivutio mbali mbali vya kitalii.

Kwa muda mrefu Wilaya ya Micheweni ilikuwa imesahaulika katika shuli mbali mbali, lakini kwa sasa Wilaya hiyo imekuwa ni moja ya Wilaya muhimu kwa upande wa Kisiwa cha Pemba, huku ikiwa inategemewa kwa kiasi kikubwa na Serikali.

Shughuli za wananchi wa Wilaya hiyo ni Kilimo, Uvuvi, ubanjaji wa Kokoto, ufugaji wa mbuzi, kuku na ngombe, huku watu wengi wakiifahamu kwamba Wilaya hiyo ni moja ya Wilaya zilizoko Ukanda wa mashariki.

Katika miaka 50 iliyopita Wilaya hiyo ilikuwa ni moja ya Wilaya iliokosa huduma mbali mbali za kijamii, ikiwemo Hospitali, skuli hata nyumba za kulala wageni.

Wananchi wa Micheweni huduma ya matibabu wakilazimika kuzifuata Wilaya ya Wete, tena kwa kutumia usafiri wa Punda kwa kipindi hicho, nyumba za kulala au kupumzikia wageni kwao ilikuwa ni kitu adimu sana.

“Micheweni ilitupwa katika kipindi cha ukoloni, ilikuwa hakuna chochote, spitali, skuli, watu wa micheweni kufuata huduma hulazimika kusafiri kwenda wete”.

Naweza kusema Wilaya ya Micheweni, ni moja ya Wilaya iliyojaaliwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii, ni moja ya Wilaya iliyopata hadhi kubwa ya kuwepo kwa mahoteli mengi na makubwa ya watalii.

Moja ya Vivutio muhimu vya Utalii vilivyoko katika Wilaya hiyo, uwepo wa msitu wa Ngezi, msitu uliojaaliwa kuwa na miti mikubwa na mirefu,huku ukiwa na urefu wa Hekta 3000-2900, msitu uliojaaliwa kuwa na wanyama wa aina mbali mbali.

Tayari msitu huo umejaaliwa kuwa na wanyama ambao wanapatikana Kisiwani Pemba tu, hakuna sehemu nyengine yoyote duniani inayoweza kuwapata wanyama hao, huku kukiwa na aina 30 za wananyama wanapatikana ndani ya mstu huo, huku kukiwa na aina mbili tu za wanyama ambao ni adimu na hawawezi kupatikana sehemu nyengine yoyo duniani.

Wanyama hao adimu na wamekuwa ni kivutio kikubwa cha wageni wengi au watalii na kulazimika kutembelea msitu huo ni pamoja na Popo wa Pemba (Pemba Flying Fox) na Paa wa Pemba (Pemba Blue Duiker). Msitu huo wa ngezi umejaaliwa kuwa na aina 131 za ndege, huku aina nne tu za ndege ndio wanaopatikana Kisiwani Pemba katika msitu huo.

Ndege hao adimu wanaopatikana katika msitu huo wa Ngenzi tu, Kihodi (Pemba Scops Owl), Ninga (Pemba Green Pegur), Manja (Pemba White Eye) Chozi Kijibiri (Pema Violeti Poreastel Sun Bird) ndege hao ni pemba tu
wanapopatikana.

Msitu huo umebahatika kuwemo kwa ndege wanaohamahama, ambao wanapatikana Pemba na nje ya nchi kama vile Madagaska na maeneo mengine ya Kenya, ndege wenyewe ni Kidonati(Madagasca Bee Eater), African Otpen Billed Stock, Mourab Stock, Water Commorant.

Katika msitu huo umebahatika kuwemo kwa aina 78 za Vipepeo, vikiwemo vipepeo adimu, vipo vinavyopatikana kisiwani Pemba katika msitu huo tu na vipo vinavyopatikana sehemu nyengine, Acrea Agina Pemba Nus.

Kivutio chengine ni Rasi kiuyu na msitu mkubwa wa micheweni, huku shehia saba (7) za wilaya hiyo zikiwa zinahifadhi misitu ya mikandaa, ili kuweka mazingira mazuri ya Wilaya.

Kuwepo kwa mnara wa kigomasha mnara ambao ulijengwa 1919, kwa sasa ukiwa na zaidi ya miaka 100, mnara huu ni moja ya minara mikubwa ya kuongozea meli, licha ya kuwa na umro mkubwa ukiangalia Teknollojia
yake iliyotumika kwa ujenzi.

Bado mnara huo unaendelea kutumika kwa kuongoza vyombo vya baharini kwa ukanda wa Africa Mashariki na kati, huku ukiwa kivutio kikubwa cha utalii kutokana na teknolojia yake iliyotumika katika ujenzi wake.

Uwepo wa Fukwe mbali mbali katika wilaya hiyo, mfano fukwe za Vumawimbi, Fukwe za mbuyuni, mapango ya kihistoria kama Panga Hatoro, huku wageni mbali mbali wakimiminika katika fukwe hizo.

Wilaya hiyo imejaaliwa kuwa na hoteli nyingi za kitalii, ambapo kwa sasa zipo tatu zilizokamilika na zinazotoa huduma, huku kukiwa na hotel inane bado ujenzi wake unaendelea.

Kuwepo kwa Chumba cha chini ya bahari ni moja ya kivutio kikubwa katika ukanda wa Africa Mashariki, huku kikiitambulisha Kisiwa Cha Pemba duniani kote.

Chumba hicho kwa siku ni US Dola 1500 tu, hoteli zote zikiw ana Vumba zaidi 55, vikiwa na vitanda 116 vya kulala wageni, baada ya mwaka mmoja kutakuwa na vyumba 200 baada kumaliza hoteli hizo.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Abeid Juma Ali, alisema utaali unaofanywa micheweni ni utalii unaoangalia hifadhi ya mazingira, kabla ya ujenzi Serikali hufanya tathmini ya mazingira, ili kulinda rasilimali ya mazingira iliyopo.

Utalii huo pia umezingatia Tamaduni, mila na desturi za wananchi wa Wilaya hiyo, ili kuhakikisha mila na tamaduni za mzanzibari zinabakia kama zilivyo.

Sekta ya Utalii ndio moja ya sekta inayoongoza katika uchumi wa Zanzibar, hivyo wananchi wengi wakaazi wa Wilaya hiyo tayari wameweza kupata ajira katika hoteli hizo za kitalii zilizoko ndani ya Wilaya hiyo.

kuwepo kwa Utalii katika Wilaya hiyo, Serikali imekuwa ikipata mapato yake makubwa, ukilinganisha na kitu chengine chochote kile. Idadi ya Watalii wanaingia Zanzibar imeongezeka kutoka 132,836 mwaka 2010 hadi kufikia 310,500 kwa mwaka 2014, huku chumba cha chini ya bahari kikitembelewa na watalii wengi kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

Kutokana na kukamilika kwa mahoteli ya kitalii Zanzibar yenye hadi ya daraja la kwanza, hoteli za nyota tano kuongezeka kupatapeleka idadi watalii kuoongezeka kutoka 310,500 mwaka 2014 hadi kufikia 500,000
mwaka 2020, huku ajira  nazo  kuongezeka kufikia 100,000.

Ujio wao umeweza kusaidia mambo mbali mbali kupata la Serikali limeongezeka, huduma mbali mbali zimepatikana ikiwemo barabara kujengwa, hospitali, na huduma nyengine za kijamii ikiwemo elimu.

Kuwepo kwa hoteli hizo katika wilaya ya Micheweni imeweza kuwapatia ajira vijana wa Wilaya hiyo, ikiwemo kufanyakazi, wakulima kuuza mazao yao hotelini huko, wavuvi kuuza samaki wao, ambapo yari vijana zaidi ya 156 wameajiriwa katika nyanja mbali mbali kwenye hoteli hizo.

Utalii unaofanywa Micheweni umekuwa ukitegemea wageni zaidi, jambo ambalo linarudisha nyuma huku mwamko wa wananchi ukiwa mdogo katika uwatii wa ndani.

“Kuna baadhi ya wananchi hata msitu wa ngenzi Utalii unaofanywa Wilaya ya micheweni unategemea wageni, wananchi wa ndani ya nchi mwamko wao ni mdogo katika kutembea maeneo mbali mbali ya watalii, kujitokeza
kwenda ngezi, kigomasha, msitu wa rasi kiuyu.

Taasisi zinazohusika na ukusanyaji wa mapato kufanya kazi zao vizuri, suala la kuchukuwa pesa za serikali mtu zitamtumbukia nyongoni, kila sekta kufanya kazi kwa wakati wake.hata hivyo alisema Sekta ya Utalii ni muhimu sana hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kulinda amani na utulivu iliyopo nchini, ili kwani amani ikivunjika hakuna litakalokuwa, ikizingatiwa sekta ya utalii ni mkombozi kwa wazanzibari, mdhamini wa Kamisheni ya Utalii Kisiwani Pemba, Suleiman Amour Suleiman alisema kwa Pemba unapozungumzia suala la Utalii lazima moja kwa moja uiguse Wilaya ya Micheweni, ambako ndiko sekta ya utalii ilikojikita zaidi.

Wilaya hiyo imepata bahati hiyo kutokana na kujaaliwa kuwa na fuke nyingi zenye kuvutia wawekezaji, huku bado zikiwa katika mazingira mazuri ya kutokuharibiwa.

Utalii katika wilaya hiyo umepiga hatua kubwa, sio kuitangaza Wilaya hiyo bali hata Pemba nzima, kwani dunia nzima tayari inafahamu Chumba cha chini ya bahari kipo Micheweni na sio Wilaya ya Mkoani.

“Wilaya yenye vivutio vingi vya kitalii kwa upande wa pemba, Msitu wa ngezi umeendelea kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa, miti maarufu ni mgomba kofi ambao unapatikana msituni hapo tu, fukwe safi na refu zenye kuvutia Pemba, ikiwemo ufukwe wa Vumawimbi, mapango mengi ya kistoria kivutio vikubwa, mnara wa kigomasha” Alisema.

Kuwepo hoteli nyingi kubwa kubwa, ukiachia Fundu lagoni iliyoko Wambaa Wilaya ya Mkoani, Micheweni ndio eneo pekee linaloitangaza Zanzibar kupitia chumba cha chini ya bahari, unalala na samaki na unaamka na samaki, katika siku 360 kinabukingi ndani ya mwaka mzima.

Hilo linatihibitishwa na Takuwimu za bungi za watalii wanaofika Pemba, kwani tayari hizi sasa Disemba kimeshakuwa na oda ya wageni kulala katika Chumba hicho hadi Febuari Mwaka 2017, hakuna siku Mtu aliyokuwa halali katika Chumba hicho.

Sekta hiyo imeweza kutoa ajira kwa vijana wa wilaya hiyo, wapo wanauza bidhaa za mboga mboga, wavuvi kuuza bidhaa zao za baharini, huku kukiwa na miradi takribani minane inatarajiwa kuanza ujenzi wake katika Wilaya hiyo zikiwemo hoteli za madaraja ya kwanza.

Dawa Juma Mshindo (75) ambaye kwa sasa ni sheha wa shehia ya Micheweni, anasema vijana na wananchi wa Micheweni “Usizarau Dafu, Embe ni tunda la matokeo”.

Huwezi kuzungumza na sheha huyu bila ya kukuachia misemo yoyote ya Kiswahili, nimetumia dakika 10 kuutafakari msemo huu na kushindwa kupata jibu, lakini zaidi aliwakusudia vijana na jamii iliyopo sasa.

Dawa ni mmoja ya wazee waliozaliwa katika Wilaya ya Micheweni na anaifahamu vilivyo Micheweni, alizaliwa mwaka 1941 katika kijiji cha Micheweni, alisema  Wilaya ya Micheweni ilikuwa nyuma kwa kila kitu.
Micheweni ni moja ya Wilaya iliyosahaulika katikla kipindi cha wakoloni, kwa kukosa huduma mbali mbali za kijamii, ambazo wananchi walipaswa kuzipata.

Anasema wananchi wa micheweni walikuwa wakilazimika kutumia usafiri wa Punda, kutoka Micheweni kwenda Wete kufuata matibabu na huduma nyengine.

Tokea kipindi hiko Wilaya ya Micheweni imekuwa ikibabadilika siku hadi siku, hadi kufikia Wilaya moja muhimu katika Kisiwa Cha Pemba na Zanzibar kwa ujumla katika sekta utalii.

Sheha Dawa anasema Micheweni imepata faida kubwa, kupitia sekta ya utalii kwa kupokea wageni siku hadi siku, kuitangaza Pemba kupitia hoteli zilizoko Makangale na magofu mengi ya kumbukumbu.

Licha ya kuwa na mahoteli mengi lakini kumejaaliwa kuwa na magofu au mapango mengi ya Kiutalii, likiwemo Pango Hatoro ambalo watafiti mbali mbali hulitua kufanya utafiti wao.

Anasema utalii ulipokuja baadhi ya wananchi walikuwa wakiuogopa, sasa hivi asilimia 75 wamepata ajira kupitia kilimo chao na uvuvi, utalii umejikita katika kusaidia wananchi  na kujenga skuli ya Mnarani.

Aliwataka wananchi kuhakikisha wanalinda Mila na Desturi za wananchi wa Micheweni, hivyo aliwataka mameneja wa mahoteli kuhakikisha wanawafahamisha wageni wao juu ya mila na desturi za wananchi wa wilaya hiyo, ili sekta hiyo iendele kuwepo na kuipatia tija Zanzibar.

Mmoja wa wekezaji wakuba Kisiwani Pemba, Meneja wa Hoteli ya Manta Resorty and Under Water Room, MNatthew Saus, alisema ni miaka 10 sasa tokea kuekeza Pemba katika sekta ya Utalii.

Anasema Pemba kwa sasa wanaishi kama ndugu wa familia moja na wananchi wa Makangale, chumba cha Chini ya Bahari kikiwa kimeipatia sifa kubwa na kupata Tunzo kwa Uponde wa African.

Chumba hicho ndio Chumba cha kwanza kuwepo bahari kwa Africa, huku kikiwa na oda ya muda mrefu kutoka kwa wageni, mikakati yao kujenga chumba chengine cha chini ya bahari mwaka ujao, kwani Chumba hicho
kimeutangaza kwa kiasi kikubwa utalii wa Zanzibar dunia.

Wafanyakazi wa mahoteli nya Kitalii Kisiwani Pemba, hawakusita kueleza yao ya Moyoni juu ya Faida walizozipata tokea kuwepo kwa hoteli hiyo, Zuwena Salum alisema anajivunia kupata maendeleo ya kuisaidia Familia yake, kusomesha mdogo wake,pamoja na kununua kiwanja cha kujengea nyumba.

Hakusita kuwataka wanawake wenzake kutambua kwam,ba kazi ya hoteli sio kazi mbaya bali mtu anaweza kufanya na kuona kama ni kazi nyengine yenye thamani kubwa.

Paulina Loliba Lubuno alisema ni mwaka wa tatu kuwepo kwake Pemba, tayari ameshaisaidia Familia yake sana kutokana na Hoteli hiyo, huku akiwa ameanza kujenga na kununua Ngombe mmoja kwa ajili ya Kufuga. Anasema Jamii imekuwa ikiona mwanamke kufanya kazi hotenini ni uhuni, wala haipendezi kazi ya hoteni ni kama kazi nyengine tu chamsingi ni kujiheshimu kwa mtu mwenyewe, akinamama kujitokeza kufanya kazi yoyote
iliyopo ili kupata haki zao.

Khalfan Aliy Mohamed kutoka Wilaya ya MkoaI Pemba, mhudumu katika hoteli ya Manta, awali alikuwa hajuwi  chochote kinachuhusiana na hoteli, lakini kwa sasa ni muhudumu anayeweza kutoa huduma zake vizuri.

“Mimi hapa sasa ndio kama nyumbani nilikuwa hata kuongea lugha sijuwi lakini hawa ndio walionisaidia na sasa najisikia vizuri japo kuwa ni kidogo kidogo tu”alisema.

 Aliwataka Vijana wenzake kutokukata tamaa na kuchagua kazi bali kufahamu kwamba kazi zote ni muhimu kama zilivyo kazi nyengine ambazo zinastahiki kufanywa.

Mwandishi wa makala haya anapatika Email:abdisuleiman33@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.