Habari za Punde

Mlinzi wa Timu ya KVZ Jaba Amesema Amejifunza Makosa Alioyafanya.

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya KVZ, Mohammed Nassor Maulid 'Jaba' alionekana kuwatoa machozi baadhi ya mashabiki wa soka visiwani Zanzibar wiki iliyopita.


Katika pambano la kombe la Shirikisho barani Afrika KVZ iliwakaribisha wageni wao Le Messeger Ngozi kutoka nchini Burundi majira ya saa kumi alasiri uwanja wa Amaan.

Kwenye pambano hilo ambalo KVZ ilitoka na ushindi wa bao 2-1, Jaba alionekana kupata nafasi takriban nne lakini alishindwa kuwaenua mashabiki majukwaani.


Inawezekana ni kutokana na uanagenzi wa mashindano ya kimataifa ingawa mchezaji huyo alishacheza michezo mingi ya kimataifa kupitia timu yake ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).



Moja kati ya nafasi aliyopata na ambayo kila aliyekuepo uwanjani hapo alidhani ataipatia timu yake bao la tatu ni ile ya dakika ya 81 ambapo baada ya kuachia mkwaju golini aliona bora awafurahishe mashabiki kwa kuonyesha mambo ya kizungu.



Hata hivyo baada ya kuelewa kwamba mashindano hayo yapo kwa mtindo wa mtoano na siyo ligi alidiriki kuwaahidi Wazanzibari kuwa atafuta machungu yao kwenye mchezo wa marejeano.



Tayari KVZ walishawasili nchini Burundi kwa ajili ya pambano hilo litakalofanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye dimba la Prince Louis Rwagasore, Bujumbura majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki.


KVZ inahitaji kutoka na ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.