Habari za Punde

Hafla ya uzinduzi wa huduma za Zantel 4G na huduma ya Ezypesa Islamic Banking Pemba

 Waandishi wa Habari wa Vyombo mbali Mbali Kisiwani Pemba, wakishuhudia uzinduzi wa huduma ya Zantel 4G huko katika ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi Pemba.
 Wasanii wa maigizo Kisiwani Pemba, Kachara na Mwinyi Mpeku, wakisherehesha shughuli ya Uzinduzi wa huduma ya Zantel 4G na uzinduzi wa huduma ya Ezypesa Islamic Bank, iliofanyika katika Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya makonyo Wawi Pemba,


 Viongozi wakuu wa Benk ya Watu wa Zanzibar PBZ, na Benk ya Kiislamu Pemba, Ali Salim na Ali Mussa, wakijumuika na Wananchi na Watendaji wa Mtandao wa simu za mkononi ya Zantel kushuhudia uzinduzi wa huduma za Zantel 4G , iliofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi Pemba.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benk ya Pbz Zanzibar, akizungumzia mashirikiano walionayo kati ya Benki ya Kiislamu na mtandao wa Simu za mkononi Zantel na kuamuwa kuanzisha huduma ya Ezypesa kwa wateja wa
Benk hiyo.
Naibu wa  Waziri wa Miundo mbinu , usafirishaji na mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum, akizungumza na Wananchi na viongozi mbali mbali katika hafla ya uzinduzi wa huduma za Zantel 4G na huduma ya Ezypesa Islamic Banking huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Pemba, kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Balozi, Ali Abeid Karume.

Picha na Bakar Mussa -Pemba,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.