Habari za Punde

Waandishi wa habari watembelea vituo vya majaribio ya Umeme Upepo na Jua Kisiwani Pemba

 MSIMAMIZI wa Mitambo ya Umeme katika Gridi ya Taifa kutoka ZECO Kisiwani Pemba, Haji Hamad Shaame akitoa maelekezo ya mitambo ya umeme wa Gridi ya Taifa Inavyofanya kazi, wakati walipotembelea kituo cha kusambazia na kupolea umeme Wesha, katika ziara ya waandishi wa habari kuangalia vituo vya majaribio ya Umeme wa nishati mbadala Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

 WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba, wakitembelea moja ya kituo cha Majaribio cha Umeme wa Nishati Mbadala Mwambe Kisiwani Pemba, kuangalia maendeleo ya mradi huo wa nishati Mbadala.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MENEJA wa Mradi wa Nishati Mbadala Maulid Shiraz Hassan, akiwaonyesha waandishi wa habari Kisiwani Pemba, vifaa vya umeme wa Upepo vilivyomo katika mmoja wa minara ya nishati ya Umeme mbadala na matumizi bora ya Nishati, mnara huo wenye urefu wa mita 70 ulioko Mwambe Wilaya ya Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

 MSHAURI mwelekezi wa Mambo ya Habari Zanzibar Ali Rashid Salim, akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari, juu ya kuandika habari sahihi zinazohusiana na nishati Mbadala mara baada ya kutembelea vituo vya majaribio ya Umeme Upepo na Jua Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
MWANDISHI wa Hbari Mwandamizi Kisiwani Pemba, Said Mohamed Ali akitoa nasaha kwa waandishi wa habari wenzake Pemba, mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea vituo vya Majaribio ya Umeme wa Nishaii mbadala Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.