Habari za Punde

Rais Dkt Magufuli: Mabadiliko hayaepukiki CCMSTATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Dodoma                                 11.03.2017
---
MWENYEKITI wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewaeleza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa mabadiliko ndani ya CCM hayaepukiki kwani hatua hiyo itakisaidia chama hicho kuimarika zaidi.

Mwenyekiti huyo wa CCM aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), huko katika ukumbi wa Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma, ikiwa ni miongoni mwa matayarisho ya mkutano mkuu maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyia hapo kesho mjini hapa.

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Magufuli alisema kuwa mabadiliko ndani ya chama hicho ni suala la lazima.

Aliongoza kuwa CCM ni miongoni mwa vyama vikongwe katika Bara la Afrika na tayari kimeshafanya mambo mengi pamoja na mabadiliko mengi ambayo yamesaidia kukiimarisha chama hicho.

Alisema kuwa CCM ni miongoni mwa chama kikongwe katika bara la Afrika sawa na chama cha ANC ambacho kina Wajumbe 110, Chama kikuu cha siasa cha nchini China CCP, nchi ambayo ina watu Bilioni moja wajumbe wake wa NEC ni 205, hivyo mabadiliko ndani ya CCM ni ya lazima hasa ikizingatiwa idadi kubwa ya wajumbe wake wa NEC.

Hivyo, Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza kuwa ipo haja kwa baadhi ya nyadhifa ndani ya chama hicho zikapunguzwa kwa lengo la kukiimarisha zikiwemo nyadhifa za Makatibu wa CCM wa Mikoa.
Alisisitiza kuwa hatua hiyo pia, itapunguza baadhi ya migogoro ambayo huwa inatokea wakati wa uchaguzi ndani ya chama hicho.

Pamoja na hayo, Mwenyekiti huo wa CCM aliendelea kusisitiza kuwa kwa vile chama hicho ni kikubwa ni lazima kifanye mabadiliko makubwa kwa faida ya chama hicho.

Alieleza kuwa wananchi walio wengi wenye vyama na wasio na vyama wamekuwa wakijiuliza na kutafuta habari za CCM katika mkutano huo mkuu maalum wa chama hicho unaendeleaje na nini kinafanyika.

Alisema kuwa hatua hiyo ni kuonesha wazi kuwa CCM ni chama kikubwa na kikongwe hapa nchini hivyo kufanya mabadiliko ni suala la lazima.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alieleza kuwa mkutano huo wa NEC una kazi moja kubwa ya kufanya mapitio ya mkutano wa NEC uliofanyika mjini Dar-es-Salaam tarehe 13, mwezi Disemba mwaka huu kwa lengo la kuja kutoa ripoti katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.

Baada ya hapo Katibu kilikuwa na mambo manne makuu, marekebisho ya Katiba , wajumbe wote wameunga mageuzi ya kukiimarisha chama na kuhakikisha kinatoa viongozi, kimepitisha kwa sauti moja ya mapendekezo ya kanuni ya CCM kwa ujumla wake na kwa sauti moja, na hiyo imeenda sambamba na kanuni za chama hicho ikiwa ni Jumuiya zote, ratiba ya CCM,inaanza mwezi wa tatu mwishoni hadi mwezi wa 12. Pia ulipokea taatrifa ya masuala ya kimaadili unayowahusu viongozi wa chama cha Mapinduzi ambao kwa nyakati tofauti wamekeuka misingi ya uongozi na kanuni za viongozi na maadili ya CCM.

Uwamuzi uliofanyika leo umezingatia kuwa wote wanaCCM watakaokwenda kinyumea na kukihujumu na kujihusishwa na rushwa na ubadhirifu na tabia zozote zille zinazokwenda kinyume na lengo ni kuhakikisha kuwa

Leo wamechukua maamuzi kwa baadhi ya wanachama, na kuwataka kuwa meindendo yao haiwakisi imani na malengo ya CCM, na miendendo ambayo haiakisi misingi ya vhama hichio na vikao havitakuwa na ajizi ya kuchukua hatua wakati wowote, na hata katika muhtaza wa chama hicho ili kuhakikisha chama hicho kinaimarika.

Humphrey Polepole
Geska Mkasa
Agenda ni kufungua mkutano, kurekebisha

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.