Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo Afungua Hospital Nungwi ya Dr Mehta's

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Dk,Ameesh Mehta mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kituo hicho cha Afya katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo hicho kikiwa sehemu ya Hospitali ya Dk Mehta's Hospital Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit kombo akiondoa kipazia kuashiria kukifungua Kituo cha Afya cha Dr Mehta's katika Kijiji cha Nungwi Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit kombo akikata utepe kuashiria kukifungua Kituo cha Afya cha Dk Mehta's Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, kulia ni Dr Mehta's akishuhudia uzinduzi huo wa kituo chake cha afya Nungwi kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wa Nungwi na vijiji vya jirani na Nungwi.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit kombo akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa Hospital hiyo Dr Mehta's baada ya kukifungua kituo hicho akipata maelezo ya uhifadhi wa dawa katika kituo hicho 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit kombo akiwa pamoja na Dk ,Ameesh Mehta wakitembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Dr.Mehta's ilioko katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Daktari Mkuu wa Hospitali ya Dk,Mehta's,Ameesh akizungumza wakati wa ufunguzi wa Hospital hiyo ilioko katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.