Habari za Punde

Baraza la vijana nchini latakiwa kuandaa mpango kazi

Na Salmin  Juma, Pemba

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla, amesema kuna umuhimu mkubwa wa Baraza la Vijana nchini kuandaa mipango kazi utakaotoa muelekeo wa mafanikio wa baraza hilo.

Amesema bila ya baraza la Vijana kutayarisha mpango kazi shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana hayatakuepo.

Ndugu Khamis aliyasema hayo leo asubuhi huko kwenye ukumbi wa mikutano wa Skuli Ya Madungu Sekondari alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la vijana  huko Pemba wa kuandaa mpango kazi wa baraza hilo.

Amesema mpango huo utatoa ajira kwa baraza na vijana ili waweze kufanya kazi kwa uhakika na kwa ufanisi katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Aidha Katibu mtendaji wa baraza la vijana Zanzibar amefahamisha kwamba mpango huo utawawezesha vijana kunufaika na fursa zilizopo na kuwa na uwezo wa kuibua fursa nyengine.

Mkutano huo uliowashirikisha wajumbe wa mabaraza ya vijana wa ngazi mbali mbali huko Pemba pia mkutano kama huo ulifanyika jana huko katika Kisiwa cha Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.