Habari za Punde

Madawa ya Kulevya: Waziri wa Katiba na Sheria aomba Shikuba akashtakiwe Marekani


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewasilisha maombi mahakamani akitaka watanzania watatu akiwemo Ally Haji maarufu Shikuba wapelekwe nchini Marekani kujibu mashtaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Kakolaki aliwataja washtakiwa katika maombi hayo kuwa ni Ally Haji maarufu Chikuba, Iddy Mfuru na Tiko Adam.

Wakili huyo aliomba kuwasilisha ushahidi na vielelezo kisha mahakama itoe uamuzi na amri kwa washtakiwa kusafirishwa.

Hata hivyo ushahidi huo haukuweza kusikilizwa kwa sababu Wakili Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na Adinan Chitale kuomba muda wa kuupitia kabla haujasomwa mahakamani.

Hakimu Mkeha alikubali kuwapa muda mpaka kesho asubuhi kwa ajili ya mahakama kusikiliza ushahidi huo, aliamuru washtakiwa kurudi rumande.

Chanzo: Mtanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.