Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BU alozi Seif Amtembelea Mama wa Waziri Kuu Mstaaf Mizengo Pinda na Kukabidhiwa Picha ya Kuchora na Msanii Maiko Samson.

Kijana Msanii Maiko Samson akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Picha yake aliyoichora na kutumika kwenye sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi hapo Ikulu ndogo ya Mkoa huo.
Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakiwa pamoja na Mchoraji Maiko Samson baada ya makabidhiano ya picha iliyochorwa na Msanii huyo wa Mkoa wa Katavi.
Balozi Seif  Kati kati aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud kushoto yake na Naibu Waziri wake Mh. Mihayo Juma N’hunga wa kwanza kushoto wakizuru na kutoa heshima kwenye Kaburi la   Bara wa  Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda Marehemu Mzee Xavery Mizengo Pinda katika Kijiji cha Kibaoni.
Balozi Seif akimpa Pole Mjane wa Mzee Xavery Mizengo Pinda Mama yake Waziri Mkuu Mstaafu Mama Alibentina Kasanga mwenye Umri wa Miaka 87.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud akimpa pole Mama wa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda Mama Alibentina Kasanga Kijijini kwake Kibaoni.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga akimpa pole Mama wa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda Mama Alibentina Kasanga Kijijini kwake Kibaoni.
Balozi Seif  wa Pili kutoka Kulia na Mkewe wa kwanza wa kwanza kutoka Kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mama Alibentina Kasanga.Wa kwanza kutoka kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.