Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ahutubia Siku ya Urithi wa Dunia. Ngome Kongwe Zanzibar.

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba kukua kwa Utalii isiwe kisingizio cha kupoteza urithi wa ulimwengu ambao ni amana inayopaswa kuenziwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine.

Alisema uhifadhi wa mali za Kale na Urithi wa Utamaduni ni mambo yenye faida kubwa kiasi kwamba mtu asiyefikia hatua ya kuheshimu Historia yake walaamu wa Historia wanaeleza huyo ni Mtumwa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia hapo katika Viwanja vya  Ngome Kongwe ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao nao umebahatika kuwemo  katika Urithi huo.

Alisema Utalii endelevu ambao ndio chachu inayoufanya urithi wa aina zote uendelee endapo jamii kama haitojipanga vyema Historia hiyo baada ya miaka michache  itatoweka na wale watalaai na wageni wanaotegemea kuchangia mapato kupitia sekta hiyo wataondaoka.

Balozi Seif alieleza kwamba jukumu la hifadhi ni la kila mwana Jamii  kwa nafasi yake na wadhifa wake katika Dunia hii. Hivyo juhudi hizi zinapaswa kuungwa mkono na kusaidia harakati hizo kwa hali yoyote katika kusaidiana na Serikali Kuu.

Alisema ni ukweli usiofichika kwamba masuala ya uhifadhi yanastahiki kupewa umuhimu mkubwa, na haya hayawezi kufanikiwa kwa kiasi chochote bila ya uhifadhi wa Mambo ya Kale yakiwemo Majengo Asilia, Miji ya Kihistoria, Utamaduni, Sanaa na mazingira asilia pamoja na Mapango ya kihistoria.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema zipo nchi zilizoendelea kiuchumi Duniani ambazo zimejipanga vyema kwenye Sekta ya Utalii endelevu wakiendelea kulinda na kuhifadhi maeneo yao maarufu ya Kihistoria.

Balozi seif alizijata baadhi ya Nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza, Ufaransa, Japani na nyengine za China, Afrika Kusini India, Morocco, Hispania Italy ambazo licha ya utajiri wao mkubwa unaoonekana hawathubutu kuharibu urithi wao wa asili na Historia yao.

Alieleza kwamba yapo mafanikio makubwa yatokanayo na uwiano uliopo wa kiuchumi na uhifadhi wa urithi ambapo Utalii kwa sasa umekuwa kivutio kikubwa cha wageni.

Alieleza kwamba utalii wa Zanzibar unategemea sana uhifadhi wa urithi wa asili na wa kiutamaduni umekuwa ukiingiza mapato makubwa Serikali na hata watu binafsi.
“ Hapa tulipo Ngome Kongwe ni sehemu moja maarufu na muhimu kwa Historia ya 

Nchi yetu. Hivyo shime tuzidishe mashirikiano kwa nguvu za pamoja juu ya kuhami na kuendeleza urithi wetu wa Zanzibar kwa faida ya Dunia Nzima ”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zaznaibar aliuomba Uongozi wa Idara ya Makumbusho kuandaa safari maalum kwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri kutembelea Magofu ya Visiwa vya Zanzibar ili kujifunza Urithi wa Taifa hili.

Alisema ni lazima na inapendeza kuona mwana Jamii anajipangia kujifunza Historia yake jambo amablo ni maarufu kwa Mtaifa m,engine Dunia ya wananchi wake kupenda utamaduni ya kufanya ziara za ndani ambazo pia huongeza mapato ya Taifa.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar Bwana  Mohamed Bhaloo alisema Jumuiya hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wadau wa Mji huo juu ya umuhimu wa kuenzi na kutunza Mji huo wa Kihistori Duniani.

Bwana Bhaloo alisema mafunzo hayo yamewezesha kuibua Wanafunzi wapatao 400 wa fani ya ufundi walioundiwa kundi la kuhudumia matengeneo ya majengo yaliyomo ndani ya Mji Mkongwe.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar alifahamisha kwamba kipo kituo kilichoanzishwa kupitia Jumuiya hiyo cha Kihistoria ya Biashara ya Utumwa Visiwani Zanzibar.

Alisema kazi hiyo ilitanguliwa na wanajumuiya hao kuendeleza Kampeni ya upandaji miti pamoja na kuzifanyia utafiti sehemu za wazi {Open Space} ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Akitoa Salamu Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiraia ya Acra Bibi  Laura alisema Acra iliyoanzishwa Nchini Itali Mwaka 1968 imekuwa ikifanya kazi katika Mataifa mbali mbali Duniani kwa lengo la kunyanyua hali za Wananchi  na kupunguza Umaskini.

Bibi Laura alisema  kwa hapa Zanzibar Taasisi ya Acra imekuwa ikifanya kazi tokea Mwaka 2005 kwa kusaidia miradi mikubwa katika Elimu, Maji, Utalii endelezo pamoja na ujenzi wa Vyoo Maskulini.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafiri Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume akimkaribisha mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ya Siku ya Urithi wa Dunia alisema Wizara yake katikia Kitengo cha Ujenzi itaendelea kuhifadhi Majengo ya zamani  ili hadhi ya Zanzibar kuwemo ndani ya Urithi wa Dunia iendelee kubakia.

Balozi Karume alizishukuru Taasisi na washirika wa Maendeleo ndani na nje ya Zanzibar hasa  Serikali ya Mamlaka ya Oman kwa juhudi zao za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kupitia mradi huo wa Uhifadhi wa Majengo la Kihistori ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.