Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba afanya uteuzi wa masheha

Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amefanya uteuzi wa masheha wapya pamoja na kuongeza idadi ya shehia mpya katika mkoa huo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ni kwamba uteuzi huo umefanyika baada ya serikali ya mkoa kupokea ushauri kutoka Wilaya uliozingatia uwezo wa mtu kutendaji .

Aidha kwa mujibu wa sheria no 8 (1) cha sheria no 8 ya mwaka 2014, ambayo imempa nguvu kisheria Mkuu wa Mkoa kufanya uteuzi wa masheha katika eneo lake.

Masheha wapya walioteuliwa ni, Ali Khatib Chwaya ameteuliwa kuwa sheha wa Shehia ya Sellem, Ramadhan Omar Ahmed Shehia ya Kipange, Mwanaidi Khamis Alela Shehia ya Maziwani na Shabaan Salim Mtwana kuwa Shehia ya Kisiwani kwa Binti Abeid.


Wengine ni Ali Khalid Ali Sheha wa shehia ya Mzambarau Takao, Mariam Juma Ali shehia ya mlindo , Said Othman Kombo Shehia ya Chamboni , Ali Hamad Sharif Shehia ya Shanake Faki Kombo Hamad Shehia ya Majenzi pamoja na Khatib Hamad Mbwana ambaye ameteuliwa kuwa sheha wa Shehia ya Kiuyu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.