Habari za Punde

Zantel yatoa taarifa ya maendeleo kuhusu uboreshaji wa huduma zake za kisasa za simu na mtandao kwa wateja

                                                                         

Dar es Salaam, 

Katika kuleta ufanisi na ubunifu kwenye sekta ya Mawasiliano, ambayo imeleta mabadiliko kwenye maisha ya mamilioni ya Watanzania, Kampuni ya mawasiliano Zantel imeendelea kuboresha huduma za kisasa za mtandao wake ili kuhakikisha wateja wao wanazidi kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi wa 4G.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Mchakato wa kuboresha mtandao wa Zantel visiwani Zanzibar na Tanzania Bara umekua ukiendelea vizuri, kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia manufaa ya teknolojia ya simu kupitia mtandao wa simu wa Zantel.”

Uboreshaji unaoendelea utaweza kuhimarisha zaidi ubora wa mtandao wetu, huduma za intaneti za kasi zinazotumiwa zaidi kwa sasa sokoni na wateja ni hii ya 4G.”

Aidha, aliongeza kwa kusema, Uboreshaji wa maeneo yote ya Stone Town na mikoa ya Magharibi umefanikiwa. Zoezi la kuendelea kuboresha huduma hizo kwa visiwa vya Unguja na Pemba linaendelea na litakamilika ifikapo Mei mwaka huu.

Mradi mzima utagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 hadi kukamilika. Mtandao wa Zantel utaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, pamoja na mtandao utakaowafikia zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania wanaotumia huduma za simu ya mkononi zenye ubora zaidi, intaneti yenye kasi pamoja na kuboresha huduma za fedha.

Amesema mradi una lengo kufanya mabadiliko kwenye vituo vyote vya huduma za katika mitandao ya simu kwa kisiwa cha Zanzibar na Tanzania Bara kwa kufunga vifaa bora vya kisasa.

Mtandao wa Zantel unawakaribisha Watanzania wote kutumia na kufurahia huduma ya intarneti ya 4G kutoka Zantel kama kampuni ya mtandao wa simu ya kwanza kuleta huduma za kibenki kwa jamii ya Kiislamu na kwa nchi nzima.

Kuhusu Zantel

Mtandao wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni miongoni mwa wawekezaji na wagunduzi kwenye sekta ya mawasilino wakiongoza kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja. Lakini zaidi ya yote, ni miongoni mwa kampuni ya mawasilino inayokuwa kwa kasi kubwa na inayotengeneza faida kubwa katika Sekta ya mawasiliano Tanzania. Mtandao huu wa Mawasiliano Zanzibar ndiyo mtandao pekee wa huduma za mawasilino unaotoa huduma ya simu za nje kwa bei nafuu, simu nab ado kupitia mfumo bora wa CDMA, GSM, 3G networks.

Huduma za Zantel zimekuwa zikikua kutokana na kuongezeka watumiaji wake huku ikizidi kuonyesha ubora katika huduma zake ambazo kila mtu anaweza kuzimudu pamoja na kutoa huduma ya haraka ya mtandao wa wireles kwa haraka na ubora.

Zantel imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi kwenye sekta ya mawasilino. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health. Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele kupata tarifa kwa haraka.
Kwa maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.