Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Afungua Itikafu na Kuzindua Jumuiya ya JUKUWAZA Zanzibar.

Naibu Mufti wa Zanzibar akisoma dua kabla ya kuaza hafla ya Uzinduzi wa Itikafu na Uzinduzi wa Jumuiya ya Kusaidi Wagonjwa na Ustawi wa Jamii Zanzibar (JUKUWAZA) iliyoanzishwa na Wanawake kwa ajili ya kusaidia Jamii uzinduzi huo umefanyika katika msikiti wa Ijumaa Muembeshauri Zanzibar. 
Mshereheshaji Ndg Khamis Ahui akisoma ratiba ya utaratibu wa hafla hiyo iliofanyika katika msikiti Mkuu wa Ijumaa Muembeshauri Zanzibar.
Sheikh Sharif akisoma Quran Tukuf kabla ya kuanza kwa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Itikafu na Jumuiya ya JUKUWAZA. 
Sheikh Mziwanda akitowa tafsiri ya Aya za Quran iliosomwa wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Itikafu na Jumuiya ya JAKUWAZA katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Muembeshauri Zanzibar.
Naibu Katibu wa Jumuiya ya Kusaidia Wagonjwa ya Ustawi waq Jamii Zanzibar JAKUWAZA  Ndg. Ali Juma Ali akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa uzinduzi wake rasmin uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud, uzinduzi huo umefanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Muembeshauri Zanzibar. 
Naibu Mufti wa Zanzibar akitowa nasaha zake kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kufungua Itikafu na Jumuiya ya JUKUWAZA Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe, Ayoub Mohammed Mahmoud akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa ufunguzi wa Itikafu ya Siku moja ilioendana na Uzinduzi wa Jumuiya ya Kusaidia Wagonjwa ya Ustawi wa Jamii Zanzibar, ikiwa na malego ya kusaidia Jamii Wajane Watoto na Wagonjwa na kuazisha Mfuko wa Dhamira ya kwenda Makka Kuhiji kwa kuchangia na kutowa fursa kila Mwanachama kupata nafasi hiyo.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakifuatilia uzinduzi huo 





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.