- Aanika
matamu, machungu ameshawahi kuvamia jimbo
NA HAJI NASSOR, PEMBA
KUTOKANA
na umahiri wangu wa kazi na kutekeleza vyema majukumu yangu, ndio maana
nikachaguliwa na kupewa hii nafasi.
Nasema haya
sikama najisifu, au kutaka sifa na kujinyoonesha kwa watu kama nayaweza, lakini
nasema haya kwa kujiamnini, na walio wengi wanaamini kama kweli mimi najiamini
na naweza.
Hizo ni
baadhi ya kauli za mwanamke mahiri ambaye anaoneka kweli anaweza na anajiamini.
Jina lake
hasa ni Tatu Abdallah Msellem, aliyeshika wadhifa wa Mwenyekiti katika Jumuiya
ya ‘Tumaini jipya’ TUJIPE kisiwani Pemba.
Mwanamke
huyu mahiri, ana historia ndefu katika maisha yake, licha ya kuwa amejinyakulia
wadhifa huo bila ya yeye mwenyewe kujua.
Kitu pekee
kilichosababisha kujinyakulia wadhifa huo, ni kutokana na kujiamini kwake
katika utendaji wa kazi na majukumu yake.
Ama kweli….
wanawake laiti kama sikujengewa, misingi potofu na ya kuwakandamiza leo,
tungewakuta kama Bi Tatu wapo kwa wengi.
Jumuia hii
‘Tuamini jipya’ anayoingoza mwanamke huu, ikiwa na akina baba 15, ilianza kazi
zake, mwaka 2008 na kupata usajili mwaka mmoja baadae.
‘’Lengo hasa
la kuanzishwa kwa Jumuiya hii ni kustawisha na kuimarisha maendeleo endelevu ya
wanajamii wa Pemba katika nyanja zote’’, alilieleza lengo.
Bi Tatu
akiwa muanzilishi wa Jumuia hiyo, waliamua kuanzisha huku wakiamini kuwa,
inaweza kusaidia kwa njia moja au nyengine, ili kuweza kuisadia jamii.
Jumuiya
ilianza ikiwa na wanachama 13, lakini kutokana na umahiri wa Mwenyekiti wake
mwanadada huyu, kwa kushirikiana na wenzake waliitangaza hadi sasa kuwa na
wanachama 32.
Ama kweli,
ile kauli isemayo wanawake wanaweza, haikwenda kombo…………kwa mweneyekiti huyu.
Wanaume
waliowengi wanaamini kuwa nafasi kama ya
Mwenyekiti, Katibu na hata msaidizi
Katibu, hushikwa na wanaume, ambapo kwa ndani ya Juamuia hii mambo ni tofauti.
‘’Muda mwingi naupoteza nikiwa katika harakati
za jumuiya huku nikizingatia kazi hizi ni kujitolea zaidi, unachokipata ni
kidogo mno’’, alisema Mwenyekiti.
Tatu Abdalla
Mselemu, ni mwanamke anaewawakilishi wanawake wengine kadhaa wa kisiwa cha
Pemba, na kuwaonyesha wale wanaume wanaodhani kuwa mwanamke hawezi kuongoza
nafasi za juu.
Mmoja wa
wasioamini kuwa mwanamke angeweza kuongoza kwenye nafasi kama hiyo ni Katibu wa
Jumuiya hiyo bw: Ali Suleiman Khamis, yeye hapa alisifu juhudi zinazochukuliwa
na Mwenyekiti wao.
‘’Unajua
kweli mwanamke anaweza tena hata kama hakuwezesha, chamsingi ni kujengewa
mazingira bora, na anaebisha aje kwenye Jumuia yetu, yupo mama mahairi Tatu
Abdalla’’,anasema.
Yeye haamini
mambo anayoyafanywa Mwenyekiti wao, kupitia Jumuia hiyo na wamefika pahala hata
kwenye uchaguzi wa mara ya pili mwaka 2011 walimpitisha kwa kura nyingi.
Inawezekana
karne kadhaa zilizopita wanawake walionekana si chohochote, na ndio maana
walikosa kutumia haki yao ya kuongoza, na leo wapo wanaokuja juu.
‘’Kwa kweli
Jumuiya nzima inamuamini Bi Tatu kutokana ukakamavu wake wa kazi zake, kiasi ambacho huweza kufanya kitu sisi
wanajumuia hatuwezi kuamini’’, alidakiza Suleiman Makame Issa ambae ni mshika
fedha.
Mshika fedha
huyu aliweka bayana kuwa, walimchaguwa mwanama
huyo aliezaliwa miaka 41 iliopita, kwa
kura nyngi za ndio, kutokana na umahiri wake.
Unaweza
kushangaa, Mwenyekiti huyu wa Jumuia ya tumaini jipya, kwamba huku ni
mfanyakazi wa serikali, wakati huo akiwa na asasi ya kimaendeleo.
‘’Walishsema
wahenga………. haba ba haba hujaza kibaba, na msemo huu kwake aliujibu kutokana na
maisha kwa sasa kumuelemea kila mmoja’’.
Mwenyewe
ansema kuwa, hapendi kuona jamii hasa kwa yale makundi yaliotajwa kuwa yako
pembezoni, kukosa haki zao kama vile za kujiamualia mambo yao na ndio maana
lengo moja la jumuia yake ni kuwakomboa .
‘’Mimi
niliishauri kamati yangu tendaji kabla hata ya kupata ufadhili, tuende baadhi
ya vijiji kukutana na wajane kuwapa elimu na hili lilipita’’,alisema kwa
ukakamavu.
Uchesi na
ukakamvu wa mwanamama huyu, amekua kama chumvi ndani ya Jumuia yake, kutokana
na kila anachokieleza, hukubalika na kisha kuzaa matunda.
Majukumu ya
Mwenyekiti huyu ni sawa na yale ya Mwenyekiti mwengine hata akiwa mwanamme,
katika Jumuia nyengine, ingawa zipo asasi za kirai kutokana na kurithi mifumo
dume, huwakosesha nafazi wanawake.
‘’Mimi majukumu yangu hasa katika Jumuiya, ni
kuhakikisha Jumuiya inatimiza malengo yake kama ilivyojipangia katika katiba’’,
alifahamisha Bi Tatu.
Jukumu
jengine na kubwa ni kutekeleza kazi nyengine za Jumuiya, kama atakavyopangiwa
na kamati Tendaji na mkutano mkuu.
Miaka hiyo
akiwa skuli alidhani suala la uongozi ni zito na hata kutafsiri kwamba,
asingeweza chohote hata kama akipewa nafasi.
Leo mwanamke
huyu ambae pia ni mfanyakazi wizara ya habari Kisiwani Pemba, anajivunia
kuongoza kundi kubwa la wanaume kwa ufanisi.
Kutokana na
umahiri wa Mwenyekiti tayari Jumuiya walishapata mradi mmoja wa mafunzo ya
utunzaji wa fedha uliofadhiliwa na Foundation for Civil Socierty.
‘’Mradi huu
ulikuwa wa miezi mitatu, uligharimu shilingi milioni saba (7,000,000) na
wanachama 15 wakiwemo na wajumbe wa kamati tendaji, walipatiwa mafunzo ’’,
alieleza Mwenyekiti.
Bi Tatu
ambae ni mwenyeji wa kijiji cha Ng’ambwa kilichopo Wilaya ya Chakechake tokea
mwaka 1975, tayari ameshajinyakulia digirii yake ya masuala ya biashara na
fedha.
‘’Nilianza
kusoma skuli darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka sita mwaka 1981, katika
skuli ya msingini ya Chachani ‘’, alisema Mwenyekiti.
Kwa elimu ya
sekondari, Bi Tatu alilazimika kubadili mazingira na kuelekea skuli ya Shamiani,
ndani ya mwaka 1989 na alimaliza hapo mnamo mwaka 1992.
‘’Baada ya
kumaliza masomo yangu mwaka huo, niliamua kusomea ualimu ngazi ya cheti chuo
cha uwalimu Mkurumah Unguja kuanzia mwaka 1999, hadi kufikia mwaka
2001’’,alieleza .
Baadae aliajiriwa
na serikali, kupitia wizara ya elimu, akiwa kama Sekretary, ingawa baadae
alianza kazi ya kusomesha.
‘’Nilisomesha Pujini msingi kwa miaka mitatu
na hapo ndipo nilipopata uhamisho na kupelekwa skuli ya msingi ya Ole na hapo
nilisomesha kwa muda wa miaka kumi’’, alifafanua.
Kabla ya
kuikwaa nafasi hii ya Mwenyekiti Bi Tatu alishawahi kuwa mjumbe wa bodi ya
wadhamini, kupitia Jumuiya ya Waganga wa jadi kisiwani Pemba.
Licha ya kuwa Jumuiya inaenda vizuri katika
kuendesha shuhguli zake, lakini kuna changamoto mbali mbali zinazowakabili
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi.
Afisa katika
kamati tendaji wa Jumuiya hiyo, Hamad Hassan Chande alimsifia sana mwanadada
huyo, na kusema kuwa ni kiongozi jemedari ndani ya Jumuiya.
Wapo wengine
waliomsifia Bi Tatu, akiwemo Hadhifa Omar Khamis, anasema kama katiba yao
haikutoa maelekezo ya kubadilishana uongozi, basi Mwenyekiti wao engeendelea
daima.
“Mimi wakati
sijamjua sana niliona ni wale wanawake wa mwaka 1972, wa hewalwa bwana, kumbe
yeye ni shujaa alietimia kwenye uongozi’’,alisema.
Pamoja na
mafanikio hayo mwanadada huyo kwenye suala la uongozi, anakula changamoto
kadhaa kama vile wanajumuia yake kuwa na uwelewa mdogo wa mambo kadhaa.
Jengine
lililozaliwa na hilo ni kujikuta akibeba majukumu mengi kwa wakati mmoja ya
Jumuia, ingawa huyamudu.
Nae kama
walivyobinaadamu wengine, amejipangia malengo yake katika safu ya uongozi, kugombania
Ubunge kwa vile anatamani sana kuona wananchi Pemba wamepiga hatua kubwa ya
kimaendeleo.
Anatamani
kesho asubuhi iwe ndo mwaka 2020 ili ajitupe tena jimboni kwa mara ya pili,
maana mwaka 2015 aliingia katika Jimbo la Ole ingawa hakufanikiw akuingia
Dodom.
“Sijafa moyo
kuingia tena jimboni, na mara hii mwaka 2020 ikifika tu, kama kawaida nachukua
fomu na kupanda juu ya kiriri kuomba kura’’,anasema.
Mwanake Asha
Bakari Juma anasema wanawake aina ya Tatu ndio haswa wanaofaa kuungwa mkono
kutokana na kuoyesha moyo wa uzalendo.
Mkuu wa mkoa
wa kusini Pemba Mwanajuma majidi Abdalla akizungumza kwenye siku ya wanawake
duniani ukumbi wa kiwanda cha Makonyo alisema, kila mwanamke anayo haki ya kuwa
kiongozi.
“Mimi si
nipo hapa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa na nip eke yangu kwa Zanzibar, sasa na
nyinyi fikeni pahala msiwaachie wanaume pekee’’’,alifafanua.
Sheikh Daud
Khamis Salum wa ofisi wa Mufti Pemba anasema hakuna kipengele ndani ya uislamu
kilichomkataza mwanamke kugombea uongozi.
“Mwanamke
anayohakia na wajibu wa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya jamii, kama nafasi anayo dini
haimkatazi’’,anaeleza.
Mzuri Issa
kutoka TAMWA anasema wamekuwa wakiwahamasisha wanawake kugombea nafasi za
uongozi na sio tu kwenye jumuia hata majimboni.
No comments:
Post a Comment