Habari za Punde

Wajumbe wa Bodi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Watembelea Kisiwani Pemba.

Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya wajumbe wa bodi hiyo kufika Ofisini Kwake kwenda kuitambulisha bodi hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na wajumbe wa bodi ya Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS), wakati wajumbe hao walipofika kujitambulisha ofisini kwake
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Salam Mbarouk Khatib, akizungumza katika mkutano wa wajumbe wa Bodi ya ZBS Zanzibar, wakati wajumbe hao walipokwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali Pemba
Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Profesa Ali Seif Mshimba akibadilishana mawazo na Viongozi wa Mkoa wa Kusini Pemba, kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, kulia ni katibu Tawala wa Mkoa huo .

Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Viwanda Zanzibar (ZBS) wakiwa katika Picha ya pamoja na Biongozi mbali mbali wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba, wakiongoza na Mkuu wa Mkoa huo Mhe:Mwanajuma Mjaid Abdall.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.