Habari za Punde

Watoto wa Kike Wilaya ya Micheweni Waiomba Serikali Kuingilia Kati Ndoa za Utotoni.

Na.Bakari Mussa. Pemba.
Watoto  wa Kike katika Wilaya ya Micheweni Pemba, wameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , kuingilia kati suala la ndoa  za umri mdogo  lililoshamiri kwa baadhi ya Wananchi wa Wilaya hiyo siku hadi siku. 

Wakizungumza na mwandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema kwamba wamekuwa wakikoseshwa haki zao za msingi ikiwemo Elimu kutoka na kupewa waume wakati wakiwa na umri wa kuendelea na masomo yao.

Walisema wakiwa kama ni watoto wa nchi hii ni vyema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kusikiliza kilio chao ili kuwanusuru kuingia katika majanga ya mimba za umri mdogo sambamba na kukosesha haki yao muhimu ya Elimu kama watoto wengine.

Watoto hao walisema wamekuwa wakiwaelezea Wazee wao umuhimu wa Elimu lakini , imekuwa ni vigumu kwao kueleweka na badala yake Wazazi wamekuwa wakiwatenza nguvu na kuozesha waume wakati wakiwa wanaendelea na masomo.

“Tumekuwa na Kilio kikubwa cha kukoseshwa masomo kwa kuozeshwa waume kwa nguvu za Wazazi , kwa maana hiyo tunaimba Serikali ifanye kila inavyowezekana kutuokowa na kadhia inayotukabili siku hadi siku,” walisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba, Abeid Juma Ali, alisema Ofisi yake inalaani vikali vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwakosesha haki zao za Msingi Watoto hao ikiwemo Elimu wakati wanauwezo wa kuendelea na masomo yao .

Alifahamisha Ofisi yake imeanza kuweka mikakati kupitia Kamati za Shehia kuweza kuyaripoti mapema matendo hayo pindipo wakipata taarifa ya kufanyika ndoa za aina hiyo , ili Serikali ya Wilaya iweze kuchukuwa hatuwa za Kisheria dhidi ya Wananchi wenye utamaduni huo.

“Nitahakikisha nimezitembelea kuli zote zilizomo ndani ya Wilaya yangu , ili kujuwa ni kwa namna gani ndoa za aina hiyo zinaendelea na kukotisha tama watoto wakike,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya .

Alisema Watoto wa Kike katika Wilaya ya Micheweni wamekuwa wakikosa fursa nyingi na hivyo baadhi ya fursa hizo kuchukuliwa na wageni kutokana na utamaduni uliojengeka kwa muda mrefu wa Wazazi kuwaozesha Watoto waume kabla ya kuamliza masomo yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.