Habari za Punde

Wizara ya Katiba na Sheria Yatowa Elimu ya Serikali Mtandao Kwa Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar WAHAMAZA

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Seif Shaban, akifungua semina ya siku moja kutowa elimu kwa waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar kuhusiana na Serikali  Mtandao, inayofanyika katika wizara ya katiba mazizini Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Seif Shaban, akifungua semina ya siku moja kutowa elimu kwa waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar kuhusiana na Serikali  Mtandao,inayofanyika katika wizara ya katiba mazizini Zanzibar.kulia Mkurugenzi wa Idara ya Serikali Mtandao Shaban Haji Chum na kushoto Afisa wa Idara hiyo Bi Raya Hamza Mohammed.
Waandishi wa Habari wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA ) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya siku moja kwa waandishi wa WAHAMAZA Zanzibar kuelewa Serikali Mtandao. 
Afisa wa Idara Serikali Mtandao Bi. Raya Hamza Mohammed akitowa mada kuhusiana na Kujenga Uelewa wa Dhana ya Serikali Mtandao,wakati wa semina hiyo kwa waandishi wa habari Zanzibar, wa Maendeleo iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali Mtandao (TEHAMA) Shaban Haji Chum akizungumza wakati wa semina hiyo na kuelezea lengo la Serikali Mtandao kwa waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali Mtandao (TEHAMA) Shaban Haji Chum akifafania jambo wakati wa semina hiyo kwa waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar.





Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar Salma Said akitowa neno la shukrani kwa Idara ya Serikali Mtandao (TEHAMA) kwa kutowa elimu juu ya Erikali Mtandao na kuwajumuisha waandishi wa jumuiya hiyo.   


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.