Habari za Punde

ZANTEL Yakabidhi Msaada wa Vitabu 152 Kwa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi Zanzibar.

Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren akikabidhi vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 kwa Mkurugenzi wa chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid ukiwa ni msaada kwa chuo hicho kutoka Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin.
Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto) akikabidhi vitabu kwa Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid. na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin wakishuhudia.
Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na ufundi Haji Abdulhamid (katikati) akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada wa vitabu 152 vyenye thamani ya Tsh 10 milioni kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour, Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour (kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi katika hafla ya kukabidhi vitabu 152 vilivyotolewa na Zantel kwa Chuo hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.