Habari za Punde

Ijitimai ya Kimataifa Zanzibar Katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Sheikh Salum Msabaha akiwasilisha Mada yake inayozungumzia Elimu katika Uislamu akitowa wakati wa Ijitimai ya Kimataifa iliowakutanisha waislamu kutoka Nchi za Afrika Mashariki na wenyeji wa Unguja na Pemba inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakifuatilia Mada zinazowasilishwa wakati wa hafla hiyo ya Ijitimai ya Kimataifa iliowakutanisha waislamu kutoka katika Nchi za Afrika Mashariki.
Sheikh Yussuf Diwani akiwahutubia na kuwasilisha Mada yake inayozungumzia Faida ya Afya katika Sala za Usiku kwa waumini hao wakati wa ijitimai hiyo. 
Sheikh Suleiman kutoka Kituo cha Redio Quran Jijini Dar es Salaam akitowa Mada wakati wa Ijimai hiyo kuhusiana na Makuzi katika Uislamu akitowa Mada yake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaohudhuria Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika Zanzibar katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akifurahia jamba wakati akizungumza na Naibu Mufti wa Malawi Sheikh Shaibu Ibrahim wakati wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.