Habari za Punde

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Atembelea na Kukagua Maeneo Yaliyoathirika na Mvua Kisiwani Pemba

 GARI aina ya kijiko kikiondoa udongo ulioporomoka na kuvunja ukuta wa ghala la kuhifadhi karafuu Mkoani, kufuatia mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha karafuu zilizokuwemo kuathirika, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 KATIBU Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Joseph Abdalla Meza (katikati) akizungumza na Mdhamini wa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi, kufuatia ghala la kuhifadhia karafuu Mkoani kuvunjika kwa kuelewa na mlima, kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 KULIA ni Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akielezea athari za mvua zilizojitokeza wilayani mwake, kwa Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Joseph Abdalla Meza (katikati) wakati alipokuwa na ziara ya kuyatembelea maeneo na nyumba za wananchi waliokumbwa na athari za mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MLIMA uliokaribu na ghala la kuhifadhi karafuu Mkoani, ambao uliporoka wiki iliopita, na kusababisha athari kwa kukatika ukuta wa ghala hilo, na karafuu zilizokuwa zimehifadhiwa kuharibika, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 KATIBU Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Joseph Abdalla Meza, mwenye mwemvuli akiangalia nyumba na msikiti ulivyokumbwa na athari ya kuelemewa na mlima, shehia ya Mbuyuni wilaya ya Mkoani Pemba, wakati wa ziara yake ya kuyatembelea maeneo na  nyumba za wananchi, zilizoathiriwa na mvua, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MSIKITI wa waumini wa shehia ya Mbuyuni wilaya ya Mkoani Pemba, ambao ni miongoni mwa majengo yaliokumbwa na athari za mvua, kwa kuangukiwa na mlima na kisha tawi la mti, ambapo kwa sasa umehamwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MITI ya aina mbali mbali ikiwemo mikarafuu, mifenesi, migomba na misheli sheli inayomilikiwa na wananchi wa kikiji cha Kwachangawe wilaya ya Mkoani Pemba, ikiwa imekatika katika, kufuatia upepo wa kasi uliovuma juzi Mei 8, pia ulisababisha nyumba sita kupata athari, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa wilaya ya Mkoani Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akimuonyesha miti iliokatika kwa upepo eneo la Kwachangaawe wilayani humo, Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Joseph Abdalla Meza, wa pili kulia, wakati Katibu mkuu huyo na ujumbe wake ulipoyatembelea maeneo kadhaa ya wananchi yalioathirika na mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba). 

NYUMBA inayomilikiwa na mwananchi Salim Saleh Mbaruok wa Kwachangaawe wilaya ya Mkoani, ikiwa imepata athari kufuatia upepo wenye kasi, uliovuma juzi na kusababisha wananchi sita nyumba zao kuharibika, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.