Habari za Punde

Wajasiri amali wadogowadogo waiomba serikali kuendelea kuwapatia elimu

Mwandishi wa habari hii wakati akimuhoji mmoja wa wajariamali wadogowadogo

Na Ali Ngome Ali, Pemba

Wajasirimali wadogo wadgo Kisiwani Pemba wameiomba Serekali kuendelea kuwapatia elimu ili kuweza kukuza mitaji yao.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizri mapema leo hii wajasiriamali hao wamesema kuwa kupatiwa nafasi za kushiriki katika mafunzo mbali mbali kunawezesha kujenga uzoefu wa biashara wanazozifanya nakuweza kujikwamua hali ngumu za kimaisha.

Time Hamada Saidi mkaazi wa Shumba ya Mjini Wilaya ya Micheweni amesema  kuwa ameweza kufanya shughuli zake za ujasiriamali kupitia mafunzo ambayo ameyapata kutoka katika taasisi mbali mbali za kiraiya na kiserekali.

Amefahamisha kuwa kupitia mradi wa GAWE umemuwezesha kujua kutunza kumbukumbu jambo ambalo awali  hakuweza kufikiria kabisa juu ya utunzaji huo.

Nae Fatma Khamis Ameir Mkaazi wa Wete amesema ipo haja kwa wajasiria mali ambao wemepata mafunzo kuweza kuyatumikia vyema kwa lengo la kuimarisha biashara zao nakuondokana nadhana yakuwa mafunzo niyakujipatia fedha pekee.

Aidha ametoa wito kwa wajasiriamali kutokuvunjika moyo nabadalayake kujiendeleza na kuondokana na hali ngumu ya kimaisha  huku wakijua biashara nikitu gani jambo ambalo litamuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.