Habari za Punde

Makocha kutoka Zanzibar wanaofundisha Ligi Kuu Bara wawafungulia njia makocha wengine

Kocha wa Stand United, Hemed Morocco

Wengine wane wanahitajika

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Idadi ya makocha kutoka Zanzibar kufundisha ligi kuu soka Tanzania bara huenda ikaongezeka msimu huu mpya wa mwaka 2017-18.

Taarifa za uhakika tulizozinasa mtandau huu kuna makocha wengne 4 huduma zao zinahitajika kwenye vilabu mbal mbali vya huko Bara.

Hayo yote yamekuja baada ya makocha wa kutoka Zanzibar msimu ulopita kufanya vzuri katika ligi hiyo na kuziweka salama klabu zao kubakia kwenye ligi hiyo.

Makocha hao wa Zanzibar waliyofundisha vilabu vya ligi kuu ya bara na kuzisaidia timu zao kutoshuka daraja ni Ali Bushir Mahmoud “Benitez” (Mwadui FC), Abdallah Mohammed Juma “Bares” (Prisons), Malale Hamsini Keya (Ruvu Shooting) na Hemed Suleiman “ Morocco” (Stand United).

Zaidi endelea kufatilia Mtandao huu utapata kuwajua ni makocha gani hao watakaopata shavu vilabu vya ligi kuu bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.