Habari za Punde

Msaada uliotolewa na Rais Dk Shein waanza kuwafikia waathirika wa mvua za masika kisiwani Pemba


WANANCHI wa Shehia 13 za Wilaya ya Chake Chake, ambao walipatwa na maafa ya nyumba zao kuanguka katika Mvua zilizonyesha Kisiwani Pemba, wakiwa na magodoro yao baada ya kukabidhiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAATHIRIKA wa Mvua zilizonyesha Kisiwani Pemba kutoka shehia 13 zilizomo ndani ya Wilaya ya Chake Chake, wakipakia wakipakia magodori yao katika gari aina ya keri, baada ya kukabidhwa misaada hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Salama Mbarouk Khatib, akiwakabidhi saruji na bati, baadhi ya masheha wa shehia 13 zilizoathirika na Mvua zilizonyesha hivi karibuni, kwa ajili ya waathirika wa mvua hizo waliomo katika shehia zao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya Chake Chake, ambao walipata na maafa ya nyumba zao kuanguka kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni, wakipakia mifuko ya saruji katika gari baada ya kukabidhiwa na Serikali ya Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni msaada Kutoka kwa Dk Sheina.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.