Habari za Punde

Pemba watolewa hatua za makundi michuano ya UMISSETA

Na Abubakar Khatib "Kisandu"

Timu ya Soka ya Pemba leo imemaliza michezo yake yote ya kundi “A” kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tabora katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza kwenye mashindano ya UMISSETA.

Katika kundi lao hilo “A” walikuwa pamoja na timu ya Manyara, Simiyu, Arusha, Mwanza, Kigoma na Tabora ambapo wamecheza michezo 6 kwa kushinda mechi 2, sare 1 na kufungwa 3 wakijikusanyia alama 7.

Wenzao Unguja bado ni kinara wa kundi “C” wakiwa na alama 15, wakifukuzwa na Dar es salam wenye alama 13 wote wameshacheza michezo 5 na lakini timu zote hizo mbili zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.

Katika kundi hilo la Unguja lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.

Michezo mitano ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0, juzi wakaipiga Mara 5-0, jana waituguwa Mbeya 1-0, na leo wakaipiga Iringa 2-1, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 15 katika michezo 5 waliyocheza wakati lango lao limeruhusu kufungwa bao moja tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.