Habari za Punde

UNGUJA YAENDELEZA UBABE WAKE MWANZA, MECHI 4 ZOTE YASHINDA BILA KUFUNGWA HATA BAO 1

Na. Abubakari Kisandu. Mwanza. 
Bao pekee la Ibrahim Abdallah Hamad “Bakayoko” limeipa ushindi mwemba timu ya soka ya Unguja walipoichapa 1-0 timu ya Mbeya kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA), mashindano ambayo yanaendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba huko mkoani Mwanza.

Kwa matokeo hayo Unguja ndio kinara akiwa na alama 12, wakifukuzwa na Dar es salam wenye alama 10 wote wameshacheza michezo 4 na timu moja tu ya juu ndiyo inayotakiwa kukata tiketi ya nusu fainali.

Timu hizo wapo kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo Unguja wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.

Mchezo mwengine Unguja watacheza kesho Jumatatu June 12, 2017 saa 4:00 za asubuhi dhidi ya Iringa na mchezo wa mwisho watamaliza Jumanne June 13, 2017 dhidi ya Dar es salam.

Michezo minne ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0, jana wakaipiga Mara 5-0 na leo waituguwa Mbeya 1-0, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 13 katika michezo 4 waliyocheza wakati lango lao bado halijaonjwa hata bao moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.