Habari za Punde

ALEY AWEKA RIKODI KUBWA UMISSETA MWANZA, KACHEZA DAKIKA 360 HAJAFUNGWA HATA BAO 1Na.Abubakari Kisandu. Mwanza.   
Mlinda Mlango namba moja wa timu ya Soka ya Unguja Aley Ali Suleiman “Manula” ameweka rikodi ya kucheza dakika 360 bila ya kuruhusu kufungwa hata bao moja katika Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA), mashindano ambayo yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba huko mkoani Mwanza.

Aley ameweza kucheza michezo minne mfululizo katika Mashindano hayo bila ya kuruhu hata bao la Offside na inaonekana amepania kuisadia timu yake kutwaa kombe hilo.

Katika Michezo minne ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0, jana wakaipiga Mara 5-0 na leo wakaituguwa Mbeya 1-0, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 13 katika michezo 4 waliyocheza wakati lango lao bado halijaonjwa .

Mbali ya uhodari wake Mlinda mlango huyo ambae ni mchezaji halali wa klabu ya  Miembeni City pia analindwa vyema na walinzi wake imara ambao ni Ibrahim Abdallah Hamad, Abubakar Khamis, Abdul aziz Ameir Khatib, Ali Asaa Omar,  Ahmed Mohd Shaaban, Abbas Yahya na  Abdurahman Seif Bausi ambao wote kwa pamoja wakisaidiana kulinda ngome hiyo.

Mchezo mwengine Unguja watacheza kesho Jumatatu June 12, 2017 saa 4:00 za asubuhi dhidi ya Iringa na mchezo wa mwisho watamaliza Jumanne June 13, 2017 dhidi ya Dar es salam na hapo tutaona Aley ataweza kucheza dakika 540 bila ya kufungwa hata bao moja?, tusubiri tuone na tunamtakia kila la kheir.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.