Habari za Punde

Unguja yaichapa Pemba katika mpira wa wavu mashindano ya Umisseta Mwanza

Timu ya Wavu ya Pemba iliyoshiriki michuano ya Umisseta Mwanza

 Na Abubakar Khatibu "Kisandu"

Jana imepigwa  dabi ( derby) ya Zanzibar kwa upande wa  mchezo wa Mpira wa Wavu (Volleyball) timu ya Unguja dhidi ya ndugu zao Pemba katika Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba huko mkoani Mwanza, ambapo Unguja imefanikiwa kushinda seti 3-1.

Mchezo huo ulikuwa namvuto sana kwa vile ni mara ya kwanza kukutana wawili hao kwani msimu huu Zanzibar zimeshiriki kanda mbili tofauti, Unguja timu yao na Pemba timu yao, hivyo kila mmoja alikuwa anataka kuweka rikodi katika mchezo huo.

Licha ya kufungwa Pemba lakini bado wanamatumaini ya kutinga robo fainali wakati wenzao Unguja tayari wameshajihakikishia tiketi ya kucheza robo fainali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.