Na Said Abdulrahman, Pemba
MTU mmoja amefariki dunia baada ya
kuangukiwa na Gogo la mti huko Machengwe,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini
Pemba.
Akithibitisho kifo cha marehemu
huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alimtaja
marehemu kuwa ni Suleima Juma Khamis (47) mkaazi wa Utaani Wete.
Alifahamisha kuwa tukio hilo lililokea hapo
jana majira ya saa 11:30 za jioni huko katika bonde la Machengwe Wilaya ya
Wete.
Alieleza kuwa marehemu alipatwa na kifo hicho akiwa
katika shughuli zake za kukata mti aina ya mfuu kwa ajili ya kupigia tanu kwani
ni kazi yake maarufu aliyokuwa akifanya
marehemu huyo.
“Ni kweli hapo jana majira ya saa
11;30 za jioni, kuna huyu Suleiman Juma Khamis, mkaazi wa Utaani alipatwa na
kifo baada ya kuangukiiwa na gogo la mfuu wakati akijaribu kuutaka huko katika
bonde la Machwengwe,”alisema Kamanda Haji.
Alisema kuwa chanzo cha kifo cha
marehemu huyo ni kuangukiwa na na gogo hilo ambapo mti huo ulikosa muelekeo na kugonga mnazi
na baadae kumuangia ambapo marehemu
aliumia sehemu za mdomoni.
“Kwa mujibu wa maelezo daktari
aliemfanyia uchunguzi ,alisema kuwa marehemu huyo aliumia katika sehemu za
mdomoni ambapo gogo hili lilipiga,’alifahamisha Haji.
“Wito wangu kwa wananchi kuacha
tabia ya kufanya kazi mtu mmoja mmoja hasa wale wavuvi pamoja na hawa ambao
wanakata miti kwa ajili kujitafutia riziki,”alisema Kamanda Haji.
Hivyo alisema iwapo Mtu atafanyakazi
kama hizo akiwa na wenzake, wanaweza kusaidiana
hata ushauri na kuepusha majanga kama hayo.
No comments:
Post a Comment