Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Kwerekwe City Kutowa Mazoezi ya Mwisho Kwa Timu ya Kombaini ya Mjini Kabla ya Kuelekea Manyara Katika Mashindano ya Rolling Stone.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Alhamis ya July 6, 2017 kuelekea Mbulu Mkoani Manyara katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017.

Lakini timu hiyo kabla ya kuondoka itacheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Kwerekwe City, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kesho Jumatano July 5, 2017 saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao pia ndio wa kuagwa vijana hao wa Mjini kabla ya kuelekea huko Mbulu Manyara.

Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.

Mjini Unguja ndio mabingwa watetezi wa Mashindano hayo ya Rolling Stone kombe  ambalo walilichukua tarehe 9 July, 2016 siku ya Jumamosi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DAREDA ya Mkoani Manyara katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.