Habari za Punde

KLABU YA KOREA KUCHEZA NA TAIFA YA JANG’OMBE

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Klabu ya Halelujah FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Korea ya kusini kesho Jumamosi July 1, 2017 itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Jang’ombe ambayo inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar, mchezo huo utapigwa majira ya saa 9:30 ya Alaasir katika uwanja wa  Amaan.

Katika mchezo huo hakutokuwa na kiingilio chochote ambapo Wakorea wenyewe watatoa tiketi bure kwa mashabiki wote watakaofika Uwanjani hapo.

Mchezo mwengine wa kirafiki timu ya Halelujah FC itacheza na timu ya Polisi ya Zanzibar inayoshiriki ligi kuu, mchezo ambao utasukumwa Jumanne July 4, 2017 saa 9:30 Alaasir katika uwanja wa Amaan.

Hallelujah FC imeanzishwa December 20, 1980 huko kwao Korea ya Kusini ambapo jana waliwasili hapa Visiwani Zanzibar kwaajili ya kufanya ziara maalum pamoja na kupata mazoezi kwa kucheza na baadhi ya vilabu vya Zanzibar.

1 comment:

  1. Ni vizuri iwapo mataifa ya Asia kama vile Korea ya kusini kupimana nguvu na vilabu vya Afrika mathalan za Tanzania. Hivi, umoja wa binadamu unawezeshwa ipasavyo!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.