Habari za Punde

Makamo wa Rais wa ZFA Mzee Zam Afungua Kozi ya Makocha Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Makamo wa Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali leo saa 3:00 za asubuhi alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa  Kozi ya awali ya makocha wa Magilikipa, kozi ambayo imeanza leo Jumatano  July 5 na kumalizika Jumanne July 11, 2017 chini ya Mkufunzi Gwiji  Saleh Ahmed Seif “Machupa”.

Kozi hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar “ZFA” ambayo itawashirikisha zaidi ya makocha 30 kutoka Unguja na Pemba na makocha hao wakimaliza kozi hiyo watapata fursa ya kutambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”.

Machupa ni Mkufunzi pekee nchini Tanzania aliyehitimu Kozi ya CAF ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa wa ndani kozi ambayo aliisomea nchini Cameroon mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu,  Machupa pia ameshahitimu kozi ya FIFA ya Ukocha wa Magolikipa ya hatua ya juu (Advanced Level) ambayo aliipata kwenye kozi iliyofayika tarehe 01 Agost, 2016 na kumalizika tarehe 05 Agost 2016, na pia Machupa ana Leseni “B” ya Ukocha inayotambuliwa na CAF.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.