Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe Shadya Awataka Wanawake Kuchukua Tahadhari.

Na. Salmin Juma. Pemba.
Naibu Waziri Wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto Mh Shadiya Mohd Suleiman amewataka akina mama kuchukua tahadhari juu ya kubeba ujauzito wasioutegemea ili kuepusha vitendo vya uhalifu kwa watoto wachanga mara baada ya kujifungua.

Mh, Shadia ameyasema hayo kufuatia tukio la kuzaliwa na kutupwa kichanga cha siku tatu huko mzambarau takao wilaya ya Wete mara baada ya kufika hospitali ya Wete ili kukijulia hali kichanga hicho.

Amesema kitendo cha kukitupa kichanga hicho ni kukivunjia haki zake za msingi za kibinadamu hivyo ameviomba vyombo vya sheria kufuatilia kwa kina tatizo hilo na iwapo itabainika kuwepo kwa uhalifu wa makusudi kwa kichanga hicho basi sheria ichukuwe mkondo wake kwa wahusika wa tukio hilo.

Aidha amesema amefarijika kuona kwamba kichanga hicho kinaendelea vizuri na kuahidi kwamba wizara yake itahakikisha kichanga hicho kiko katika hali ya usalama na akiwa chini ya uangalizi wa mama ake mzazi ili aweze kupata haki zake za msingi ikiwema ziwa la mama.

Nae mkuu wa kitengo cha uzazi wa mpango na Afya ya uzazi bibi Sharifa Homoud Rashid amesema hadi mda huu hali ya mama na mtoto inaendelea vizuri na wanahakikisha wanafuatilia maendeleo ya afya yake kila siku ili kuona kwamba hali yakichanga hicho kinazidi kuimarika.

Hili ni tukio la pili kwa miezi ya hivi karibuni kwa vitoto vichanga kukumbwa na mikasa kama hiyo kutoka kwa mama zao wazazi ambapo moja lilitokea Micheweni kuliko zaliwa kichanga kikauliwa na kutupwa porini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.