Habari za Punde

Waziri Lukuvi na Balozi wa Japan Yoshida Wazinduwa Mabweni ya Skuli ya Idodi Iringa.

Balozi wa Japan nchini  Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi  wa  pili  kulia na wa  kwanza  kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela ,Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Balozi wa Japan nchini  Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi  wa  pili  kulia na wa  kwanza  kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela ,Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Vitanda  vilivyopo katika  bweni  hilo
Hili  ndilo  bweni la kisasa  lililojengwa na ubalozi wa   Japan  nchini
Mkuu  wa Mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akimkaribisha  balozi  wa Japan  nchini
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akizungumza na  wananchi na  wanafunzi wa sekondari ya  Idodi
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi  taa za  mionzi ya  jua  kwa mkuu  wa  shule ya  sekondari Idodi kulia  kwake ni mbunge wa  Isiman Wiliam Lukuvi na mkuu wa  wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa CCM Iringa  vijijini  Dodo Sambo
Balozi wa Japan  nchini akimkabidhi  taa hizo  mbunge wa Isimani wiliam Lukuvi
Waziri  wa  ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi  ambae ni mbunge wa Ismani akimsaidia  balozi wa Japan nchini kukaa katika  kiti  cha asili ya  Kihehe baada ya  kuvishwa  nguo  hizo za heshima
Balozi  wa Japan  nchini  akivishwa  nguo  za  kichifu  wa  wahehe
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akivishwa  nguo  za kichifu
balozi  wa japan nchini  akiwa na  nguo za  kijadi  za  kihehe  akisema hapa KAZI TU
Mkuu wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  kushoto na  waziri Lukuvi na  DC  Iringa Kasesela wakiwa na balozi wa Japan  nchini Masaharu Yoshida
Mbunge  wa Ismani na  waziri wa ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi  Wiliam Lukuvi akimpongeza  balozi wa  Japan kwa msaada  wa  ujenzi wa Bweni
NA MatukiodaimaBlog 

UBALOZI wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli. 

ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza leo  wakati wa uzinduzi wa Bweni hilo la wanafunzi shule ya sekondari ya Idodi Iringa balozi Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania. 

Alisema kuwa hatua Japan kufika kusaidia ujenzi wa bweni hilo katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliloomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali kuteketea kwa Moto.

"waziri Lukuvi lileta maombi ya mradi wa kujengewa  miradi hiyo ya maendeleo ambayo ni Hostel ya wasichana shale ya wasichana Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka2008 kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa... namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo"

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo. 

" Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji.... Hosteli hii sasa inauwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema"

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua  kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo. 

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri. 

Mbunge wa Ismani waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine bado amepongeza kwa hatua ya balozi huyu kubariki zaidi ya shilingi milioni 11 zilizobaki katika ujenzi wa bweni hilo kutumika kununua vifaa vya kusambaza maji ya kisima kitakachochimbwa shuleni hapo. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.