Habari za Punde

Waziri wa Fedha Dkt.Philip Mpango Aipongeza PPRA Kwa Kusaidia Serikali Katika Kuziba Myanya ya Manunuzi Holela Serikalini.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA) kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza wakwanza kulia, ni Meneja wa Usimamizi na Utawala wa Mifumo ya TEHAMA  wa PPRA, Bw.Bernard Ntelya na Afisa 
Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bw. Mcharo Mrutu.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, imeipongeza Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA), kwa kuisaidia serikali kuziba yanya ya upotevu wa fedha na uonevu uliokuwa ukifanywa katika manunuzi kwenye sekta ya umma, lakini akaishauri itoe elimu zaidi kwani watu wengi wakiwemo maafisa wa serikali bado hawajaelimika vya kutosha kuhusu wajibu wa kuitumia na kufuata taratibu za PPRA.
Waziri aliyasema hayo wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo ambayo inashiriki maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Dkt. Mpango alisema "Mnafanya kazi nzuri sana kwa hivi sasa, lakini mnatakiwa kuongeza juhudi katika kuelimisha kuhusu umuhimu wa kufuata taratibu za manunuzi katika sekta ya umma." Alisema Dkt. Mpango.
PPRA imeanzishwa kwa sheria ya manunuzi ya Umma CAP 410 kama ilivyobadilishwa na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya namba 7 ya mwaka 2011 ambayo inatoa Mamlaka ya kusimamia manunuzi ya umma kwa taasisi zote za Umma (Serikali), upande wa Tanzania Bara.
 Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akitazama vipeperushi vyenye taarifa za Mamlaka hiyo.

 Waziri Dkt. Mpango akiwa na Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja, (wapili kulia), wakatinakianza kutembeela banda hilo.
Meneja wa Usimamizi na Utawala wa Mifumo ya TEHAMA  wa PPRA, Bw.Bernard Ntely(kulia), akimsikiliza Mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mamlaka hiyo ili kupata ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.